Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shule ya Sekondari Savannah Plains ni miongoni wa shule zinazofanya vizuri hapa Tanzania! Shule hii ya bweni ambayo sasa inang’ara pia katika anga za kimataifa ipo Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga mkabala na barabara kuu ya Shinyanga – Mwanza!.
Hivi karibuni Savannah Plains High School ilipata fursa ya kushiriki katika mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (Johannesburg Summer Holiday Open Debate and Public Speaking Tournaments ) yaliyofanyika katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini kuanzia Desemba 11 hadi 19, 2023.
Mratibu wa Kiingereza na Mkuu wa Idara ya Lugha katika Shule ya Sekondari Savannah Plains, Josephine Kinyunyi ambaye ndiye aliyeenda Afrika Kusini na wanafunzi kwa ajili ya mashindano hayo anasema shule sita kutoka Tanzania zilishiriki lakini shule pekee kutoka Tanzania iliyoweza kufika Fainali ni Savannah Plains ikiwakilishwa na mwanafunzi Yolanda Thomas Henjelewe ambaye alikuwa mshindi wa kwanza kutoka Tanzania, mshindi wa tatu kutoka Afrika Mashariki na mshindi wa tano wa Afrika.
Walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari Savannah Plains wakiwa na wanafunzi walioshiriki mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza Afrika Kusini.
“Lakini pia katika 10 bora tulikuwa na wanafunzi wetu wanne kutoka Savannah, ukizingatia kwamba Savannah ndiyo shule pekee ya Tanzania iliyopata uwakilishi kwenye Fainali. Baada ya mashindano tulipewa Tuzo ya The Best Speaker from Tanzania, the Third Speaker From East Africa, na Fifth Speaker from Africa na kwa ujumla tulipewa Tuzo ya The Best Public Speaking School from Tanzania (The Best Tanzanian School – The Johannesburg International Summer Holiday Open – SHO”, anaeleza Josephine.
SAFARI YA KWENDA AFRIKA KUSINI ILIANZAJE?
“Tulikuwa shule sita kutoka Tanzania lakini katika Kanda ya Ziwa ilikuwa Savannah Plains High School, tulisafiri na wanafunzi 18 ambapo kati ya wanafunzi 18 tulipata nafasi ya kushiriki Afrika Kusini baada ya kuwa tumeshiriki mashindano ya Mwalimu J.K. Nyerere ya Mjadala na kuongea kwenye hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Debate and Public Speaking Tournaments) yaliyofanyika Oktoba 14,2023 jijini Dar es salaam kwa ajili ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yaliyokuwa na shule za Tanzania, Kenya Uganda na Zanzibar”,amesema Josephine.
Mratibu wa Kiingereza na Mkuu wa Idara ya Lugha katika Shule ya Sekondari Savannah Plains, Josephine Kinyunyi.
Ameongeza kuwa baada ya kuwa wameshiriki wanafunzi kwenye mashindano hayo, wanafunzi wao walifanya vizuri sana ambapo Mwanafunzi wao ambaye ni Yolanda Thomas Henjewele alishinda kwenye kipengele cha kuongea kwenye hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (Public Speaking) hivyo basi ikawa imewapa tiketi ya kushiriki mashindano ya Afrika ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza yaliyofanyika Afrika Kusini.
“Katika Mwalimu J.K. Nyerere ya Mjadala na kuongea kwenye hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza yaliyofanyika Dar es salaam,tulienda na wanafunzi 10 ambapo kati ya wanafunzi hao 10, wanafunzi wetu watano waliingia katika robo, nusu na fainali, tulivyofika Afrika Kusini tulikuwa na nchi za Afrika karibia zote ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Nigeria, Afrika Kusini, Botswana nk ambapo kulikuwa na washiriki zaidi ya 500 kutoka nchi za Afrika”,anabainisha Josephine.
“Kutoka Tanzania tulikuwa na shule sita lakini shule pekee kutoka Tanzania iliyoweza kufika Fainali na Savannah Plains ikiwakilishwa na mwanafunzi Yolanda Henjelewe ambaye alikuwa mshindi wa kwanza kutoka Tanzania, mshindi wa tatu kutoka Afrika Mashariki na mshindi wa tano wa Afrika na wanafunzi wanne kutoka Savannah waliingia kwenye 10 bora”,amesema.
Nao wanafunzi walioshiriki mashindano hayo, akiwemo Yolanda Thomas Henjewele na Allan Kabaya wamesema mashindano hayo nchini Afrika Kusini yamewapa fursa ya kujifunza na kukutana na watu mbalimbali kutoka barani Afrika.
“Mashindano yalikuwa mazuri sana,tulijifunza vitu vingi vizuri, tumepata Exposure, tumepata uzoefu wa kuongea kwenye hadhara kubwa yenye washiriki zaidi ya 500,tumekutana na wanafunzi kutoka shule mbalimbali barani Afrika, tumebadilishana mawazo,uzoefu na kujifunza vitu mbalimbali ikiwemo elimu na maisha kwa ujumla”,amesema Yolanda mshindi wa kwanza kutoka Tanzania, mshindi wa tatu kutoka Afrika Mashariki na mshindi wa tano wa Afrika.
“Tulijiandaa vizuri kushiriki kwenye mashindano, tumerudi na ushindi, tumeandika historia, tumejifunza pia masuala ya usafi na kujituma zaidi. Tunaishukuru shule hii kwa kuwapa fursa mbalimbali wanafunzi, hii ni shule nzuri ina mambo mengi mazuri”,anaongeza Mwanafunzi wa kidato cha pili Allan Kabaya aliyeshiriki mashindano hayo akiwa kidato cha kwanza.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Savannah Plains, Yona Ludomya ametoa wito kwa serikali, wazazi na jamii kwa ujumla waendelee kushirikiana na shule hiyo kwani huo ulikuwa mwanzo tu na hivi karibuni watashiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mjadala na Kuongea kwenye hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (World Championship Debate and Public Speaking Tournaments) yatakayofanyika Jijini Nairobi, Kenya.
“Kwa niaba ya Mkurugenzi wetu Hamad Hilal Hamad kwanza tunawashukuru sana wazazi kwa jinsi walivyoitikia kutuamini kwamba tupo katika utoaji elimu bora, hivyo tukachukua watoto wao kwa makubaliano tukawachukua kuwapeleka Afrika Kusini kwa ajili ya ziara ya kimasomo.Tulikwenda kushiriki na tukarudi washindi”,amesema Ludomya.
“Pia kwa niaba ya uongozi wa shule tunaishukuru sana serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ngazi zote kwa sababu taarifa hizi tulianza kuzitafutia mamlaka ya ruhusa kuanzia ngazi ya chini mpaka kitaifa. Kwa kweli tumeshirikiana vizuri sana na serikali mpaka kuwatoa wanafunzi hapa na kuwafikisha Afrika Kusini na kuwarudisha na kwa mafanikio tuliyoyapata”,ameongeza Mkuu huyo wa shule.
Katika hatua nyingine amesema miongoni mwa mambo yanayoifanya Savannah Plains High school iwe shule ya kipekee ni kwamba inaongozwa na maadili bora kwa walimu na wanafunzi, taaluma bora, mazingira rafiki ya kujifunzia kwa mwanafunzi wa aina yoyote wakiwemo wenye mahitaji maalum, malezi mazuri na huduma za afya ikiwemo lishe bora kwa walimu na wanafunzi.
Michepuo inayotolewa Savannah Plains High School ni PCM,PCB, PGM, HGE, EGM, HGL,HGK, HKL na ECA.
Kwa Mawasiliano zaidi +255 742 555 550 / 0743919187/0742919198
Mratibu wa Kiingereza na Mkuu wa Idara ya Lugha katika Shule ya Sekondari Savannah Plains ,Josephine Kinyunyi akiwa na wanafunzi walioshiriki mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (Johannesburg Summer Holiday Open Debate and Public Speaking Tournaments )
Mratibu wa Kiingereza na Mkuu wa Idara ya Lugha katika Shule ya Sekondari Savannah Plains, Josephine Kinyunyi akielezea kuhusu mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (Johannesburg Summer Holiday Open Debate and Public Speaking Tournaments ) yaliyofanyika katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini
Mkuu wa Shule ya Sekondari Savannah Plains, Yona Ludomya akielezea mambo mbalimbali yanayofanyika katika shule hiyo
Mkuu wa Shule ya Sekondari Savannah Plains, Yona Ludomya akielezea mambo mbalimbali yanayofanyika katika shule hiyo
Tuzo zilizotolewa kwa Shule ya Sekondari Savannah Plains baada ya kushiriki mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza
Tuzo iliyotolewa kwa Shule ya Sekondari Savannah Plains baada ya kushiriki mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (Johannesburg Summer Holiday Open Debate and Public Speaking Tournaments )
Mwanafunzi Yolanda Thomas Henjewele akielezea alivyoshiriki mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (Johannesburg Summer Holiday Open Debate and Public Speaking Tournaments )
Mwanafunzi Allan Kabaya akielezea alivyoshiriki mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (Johannesburg Summer Holiday Open Debate and Public Speaking Tournaments)
Walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari Savannah Plains wakifurahia tuzo za mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza
Walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari Savannah Plains wakiwa na tuzo na vyeti vya kushiriki mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza
Walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari Savannah Plains wakifurahia tuzo na vyeti vya kushiriki mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza
Walimu wa shule ya Sekondari Savannah Plains wakifurahia tuzo za mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza
Walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari Savannah Plains wakipiga picha ya kumbukumbu.
Kwa Mawasiliano zaidi Savannah Plains High School +255 742 555 550 / 0743919187/0742919198
إرسال تعليق