Jumuiya ya Wazazi yampongeza Dk. Samia kukamilisha miradi ya Kimkakati.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Haji Kianga (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa jumuiya hiyo wakishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Wazazi wilaya ya Bariadi.
 


 

Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

 

JUMUIYA ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu imempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi na Miradi ya kimkakati ikiwemo ukamilishaji wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere, Reli ya Kisasa (SGR) na Daraja la Kigongo-Busisi.

 

Aidha, ukamilishaji wa miradi hiyo, unalenga kuimarisha uchumi wa Afrika Mashariki na kati na pia miradi hiyo itaongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali, kukuza ajira na kukuza uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja.

 

Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Katibu wa jumuiya hiyo Haji Kianga wakati akiongea na vyombo vya habari ambapo aliwataka wananchi kuendelea kuunga mkono kasi ya Dk. Samia Suluhu Hassan.

 

Alifafanua kuwa, kuna mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria katika mkoa wa Simiyu umeanza kutekelezwa kwa gharama ya shilingi Bil. 444 katika wilaya za Busega, Itilima, Bariadi, Maswa na Meatu.

 

‘’Sisi tunaoishi ukanda huu, Mama ametuhurumia wana Simiyu, maji yalikuwa ya chumvi kabisa, mama anatuletea maji tuogelee kama bata…wakandarasi wameshaanza kutekeleza miradi, mradi huu utagharimu Bil. 444’’ alisema.

 

Aliongeza kuwa huduma za afya zimeimarisha kwa mkoa wa Simiyu na mikoa jirani ambapo wanawake wanapata huduma karibu na maeneo yao na pia viwanda vya kusindika mafuta ya pamba na alizeti vinajengwa ili kuongea ajira kwa vijana.

 

‘’vyungu viwili kati ya tisa katika bwawa la mwalimu Nyerere vitawashwa, hakutakuwa na hoja ya kukatika kwa umeme, Watanzania tutegemee mafanikio kwa serikali ya Dk. Samia Suluhu Hassan…Jumuiya ya Wazazi wajitokeze kugombea nafasi za serikali za mitaa na tutatoa elimu ili wajiandikishe katika daftari la wapiga kura’’ alisema.

 

Aliongeza kuwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 watatengeneza wigo mpana na kutoa elimu ili wanawake wajitokeze kuwania nafasi za uongozi kwa lengo la kupata viongozi bora wala siyo bora viongozi.

 

MWISHO.

 

Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Bariadi wakishiriki kupanda miti ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita za Upandaji miti.


Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Bariadi wakishiriki kupanda miti katika nyumba za viongozi wa CCM ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita za Upandaji miti.

 

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Haji Kianga (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa jumuiya hiyo wakishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Wazazi wilaya ya Bariadi.

 




 

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم