Na Costantine Mathias, Bariadi.
SERIKALI kwa kushikiana na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) linatarajia kutekeleza Kampeni ya Ugawaji wa Vyandarua 225,963 vyenye dawa katika Halmashauri ya wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu.
Vyandarua hivyo ambavyo vitagawiwa katika kata zote 21 na vijiji 84,
zimelenga kutokomeza Ugonjwa wa Malaria ambapo kila mwananchi atagawiwa bure
mara baada ya kujiandikisha.
Akizungumza juzi kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya ya Bariadi
Bw.Winfred Mwafongo Afisa kutoka Wizara ya Afya alieleza kuwa kampeni hiyo
inalenga kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria hivyo kupunguza vifo
vinavyotokana na ugonjwa huo.
Aidha alifafafanua kuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kampeni hii
itatekelezwa katika kila kijiji hivyo wananchi wanatakiwa kuitikia kwa
kujisajili ili waweze kupata vyandarua hivyo.
“Hii kampeni tunampa chandarua kila mwananchi lakini ili apate ni lazima aandikishwe halafu apate kuponi kusudi siku ya ugawaji anakuja na ile kuponi yake ndipo anapewa chandarua” alibainisha Bw.Mwafongo.
Alisema kuwa lengo la kugawa vyandarua hivyo ni kupunguza maambukizi ya
malaria kutoka kwa mbu mwenye vimelea kwenda kwa binadamu huku lengo lingine ni
kupunguza idadi ya wagonjwa wa malaria katika eneo husika.
Katika hatua nyingine Mwafongo aliwatoa hofu wananchi na kuwaeleza kuwa vyandarua hivyo havina madhara yoyote kwa mtumiaji, ambapo vimetolewa na serikali kwa lengo la kukabiliana na Malaria.
MWISHO.
Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bariadi pamoja na Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
إرسال تعليق