Na, Samirah Yusuph. ITILIMA.
WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, imeanza taratibu za manunuzi ili kuisaidia jumuiya ya mto Zanzui kukarabati (mota) iliyokuwa imeungua na kisababisha adha ya ukosefu wa maji.
Baada ya uwepo wa adha hiyo Meneja wa RUWASA wilaya ya Itilima Mhandisi Hussein Yahaya amesema wananchi walikosa huduma ya maji baada ya mota ya mtambo wa kusukuma maji kuungua.
"Baada ya kupokea taarifa ya mota kuungua, tulituma fundi wetu kwa ajili ya kufanya tathimini na baada ya hapo tulitafuta mzabuni wa kununua na kufunga mota hiyo ambapo tayari amepatikana na vifaa vyote vinavyohusika katika ukarabati vimenunuliwa hivyo tunasubiri vifike ili ukarabati ufanyike," Amesema Mhandisi Hussein.
Jumuiya ya mto Zanzui inajumuisha vijiji viwili ambavyo ni Zanzui na Mlimani ambapo zaidi ya wananchi 5000 wanatumia mradi wa maji Zanzui kujipatia huduma ya maji safi na salama.
Jumuiya hiyo imekuwa ikijihusisha na usimamizi wa mradi pamoja na ukarabati chini ya Ruwasa hivyo ununuzi wa vifaa hivyo vya ukarabati utanisaidia jumuiya kupunguza gharama za ukarabati ambao walitakiwa kufanya.
Mwisho.
|
|
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

إرسال تعليق