CCM kuendelea kutetea wachimbaji wadogo.


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed akiongea kwenye mkutano wa hadhara Dutwa.
 

 

Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu kimesema kitaendelea kuwatetea na kuwasimamia wachimbaji wadogo ambao wanaonzisha migodi midogomidogo ili waweze kunufaika kutokana na kuanzisha maeneo hayo.

 

Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Shemsa Mohammed kwenye mwendelezo wa ziara ya Tarafa kwa Tarafa iliyofanyika katika Tarafa ya Nkololo na Dutwa wilayani Bariadi kwa lengo la kukiimarisha na kujenga Uhai wa Chama Cha Mapinduzi.

 

Ameeleza kuwa CCM ilishatoa maelekezo kwa Afisa madini kuwapa kipaumbele wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakigundua migodi ya madini na endapo wataendelea kunyang’anywa maeneo yao, Chama na Serikali kitawasimamia kuhakikiha haki inapatikana.

 

‘’Maelekezo ya Chama na Serikali, walioanza kuchimba awali katika eneo husika wapewe kipaumbele…labda leseni iwe imeombwa miaka mingi iliyopita, na kama mmengundua na leseni ikapatikana baadae ni haki yenu kuchimba eneo hilo.

 

Aidha, Shemsa amewataka wananchi kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi na serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ili iendelee kutekeleza miradi na kuwaletea wananchi maendeleo ambapo fedha nyingi zimeletwa vijijini.

 

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo amewataka watumishi wa serikali kuendelea kutoa huduma bora katika sekta za Afya, Elimu, Maji na Umeme ili wananchi waone tija ya miradi inayoletwa na serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

Shema ameendelea na ziara ya Tarafa kwa Tarafa kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi huku akiongea na Wenyeviti wa vijiji na vitongoji, wajumbe na mabalozi wa mashina na matawi pamoja na viongozi wa dini.

 

MWISHO.

 

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed akiongea kwenye mkutano wa hadhara Dutwa.

 

Wananchi wakimpungia mkono Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed (hayupo pichani) kwenye mkutano wa Tarafa kwa Tarafa uliofanyika Tarafa ya Dutwa wilayani Bariadi.


Wananchi wa Tarafa ya Dutwa wakiwa kwenye mkutano.


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed akifurahia wakati akiingia kwenye mkutano wa hadhara Tarafa ya Dutwa.

 

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed akifurahia wakati akiingia kwenye mkutano wa hadhara Tarafa ya Dutwa.

 

WanaCCM Tarafa ya Dutwa wakiimba kwenye mkutano wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu uliofanyika Tarafa ya Dutwa.


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed akicheza pamoja na wanachama wa CCM Tarafa ya Dutwa.

 

 

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post