Kamanda Swebe awataka Askari polisi kuzingatia Weledi kazini.

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe (wa pili kulia), akiwa na baadhi ya Maafisa wa Polisi wakitoa maelekezo kwa polisi wapya (hawapo pichani) juu ya kutekeleza maagizo ya jeshi hilo.

Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe amewataka askari polisi kuzingatia haki, nidhamu, weledi na uadilifu katika utendaji wa kazi zao za kila siku katika kuwatumikia wananchi.

Hayo yamebainishwa leo na Kamanda Swebe wakati akifunga mafunzo na kuwaaga maaskari wapya 68 walioajiriwa hivi karibuni, huku akiwataka kutekeleza mafundisho kwa vitendo.

Amesema jeshi hilo linaongozwa kwa kanuni, sheria na taratibu huku akiwasisitiza kuzingatia weledi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2025.

‘’Yale waliyofundishwa wakayafanye kwa vitendo, lakini wazingatie nidhamu, haki, weledi na uadilifu katika utendaji wao…tumewaasa wazingatie haki, tutaendelea kuwa tayari na kuwajengea uwezo askari wetu’’ amesema Swebe.

Amewataka wananchi wa Mkoa wa Simiyu kuwapokea askari hao na kuwatambua kama sehemu yao ikiwemo kuwakimbilia ili waweze kutatua changamoto zinazowakabili.

Aidha, Kamanda Swebe amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Polisi (Camilius Wambura) kwa kuendelea kumimina ajira katika mkoa huo ili kupunguza changamoto katika utoaji wa huduma.

MWISHO.

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe (wa pili kulia), akiwa na baadhi ya Maofisa wa Polisi wakitoa maelekezo kwa polisi wapya (hawapo pichani) juu ya kutekeleza maagizo ya jeshi hilo.

Askari polisi wapya walioajiriwa Mkoa wa Simiyu.

Askari polisi.

Maofisa wa Polisi Mkoa wa Simiyu.

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post