Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda (mwenye shati jeusi kulia) akimsikiliza Mmiliki wa Bigone Investment Co. Ltd ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki Stanslaus Nyongo (mwenye reflectore ya mistari) mara baada ya kutembelea ujenzi wa kiwanda cha kuchambua pamba.
Na Mwandishi wetu, Maswa.
MKUU wa mkoa wa Simiyu, Dk.t Yahaya Nawanda ameipongeza Kampuni ya BIGONE INVESTMENT Co. Ltd ya Mjini Maswa kwa kuanza ujenzi wa kiwanda ili kuwekeza katika wilaya ya Maswa.
Pia amempongeza Mmiliki wa Kampuni hiyo ambaye ni Mzaliwa wa wilaya hiyo, Stanslaus Nyongo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki (CCM).
Dkt. Nawanda amesema hayo mara baada ya kutembelea eneo la viwanda lililotengwa maeneo ya Ng'hami mjini Maswa ambalo kampuni hiyo inajenga kiwanda cha Kuchambua Pamba.
Amesema kuwa serikali ya mkoa wa Simiyu inawakaribisha Wawekezaji Wazawa na wale wa kutoka nje ya mkoa na nje ya nchi ili waweze kuwekeza katika mkoa huo ambao una fursa nyingi na kwa uwekezaji kama huo unatoka Ajira kwa vijana.
Aidha amelitaka Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) kuhakikisha linafikisha umeme katika kiwanda hicho ili kitakapokamilika kinaanza kazi mara Moja.
MWISHO.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda ( wa kwanza kushoto) akisikiliza maelezo Mmiliki wa Bigone Investment Stanslaus Nyongo (mwenye shati jeupe)
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, kwa kujenga kiwanza cha Pamba, kulia ni Mkuu wa
wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda ( mwenye shati jeusi kushoto) akimsikiliza Mmiliki wa Bigone Investment Stanslaus Nyongo (mwenye shati jeupe)
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, juu ya ujenzi wa kiwanda cha kuchambua Pamba.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda ( wa kwanza kushoto) akimpongeza
Mmiliki wa Bigone Investment Stanslaus Nyongo (mwenye shati jeupe)
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, kwa kujenga kiwanda cha kuchambua pamba, kulia ni Mkuu wa
wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge.


Post a Comment