NMB yamkabidhi Trekta ya Kilimo (Powertiller) mshindi Bonge la Mpango.

Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Restus Assenga akimkabidhi zawadi ya Trekta ya kilimo (Powertiller) msindi wa kwaza wa Kampeini ya Bonge la Mpango kutoka Kahama Mkoani Shinyanga Bernad Kimario (kushoto). (wa pili kulia) Meneja Mauzo NMB Janeth Nyamko.

Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Restus Assenga akimkabidhi zawadi ya Trekta ya kilimo (Powertiller) msindi wa kwaza wa Kampeini ya Bonge la Mpango kutoka Kahama Mkoani Shinyanga Bernad Kimario (kushoto). (wa pili kulia) Meneja Mauzo NMB Janeth Nyamko.

Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Restus Assenga akimkabidhi zawadi ya Jiko la Umeme msindi wa pili wa Kampeini ya Bonge la Mpango kutoka Kahama Mkoani Shinyanga Chausiku Tindiga, ambaye zawadi yake ilipokelewa na mwakilishi wake  Hassan Abuduly (kushoto). (wa pili kulia) Meneja Mauzo NMB Janeth Nyamko.




Na Derick Milton, Kahama.

Wateja wa Benki ya NMB wameendelea kujipatia zawadi mbalimbali zinazotolewa na beki hiyo kupitia kampeini yake ya Bonge la Mpango, ambapo jana Bernad Kimario mkazi wa Kahama Mkoani Shinyanga amekabidhiwa trekta ya kilimo (Powertiller) baada ya kuibuka mshindi.

Hafla ya kukabidhi zawadi hiyo imefanyika mjini Kahama, ambapo mbali na mshindi huyo Benki hiyo ilimzawadia jiko la umeme Chausiku Tindiga mkazi wa Shinyanga ambaye aliibuka mshindi wa pili kwenye kampeini hiyo.

Wateja hao waliibuka washindi katika droo hiyo iliyochezeshwa na Benki hiyo katika wiki ya nane ya kampeini hiyo, ambapo walikabidhiwa zawadi hizo na Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Restus Assenga.

Mbali na kukabidhi zawadi hizo, Benki hiyo iliendesha droo ya kumi ya kampeini hiyo ambapo Kalinga Hassan kutoka mkoani Mwanza, alibuka mshindi wa kwanza na kujishindia zawadi ya trekta ya kilimo (Powertiller).

Droo hiyo ambayo iliendeshwa na Meneja mauzo NMB Janeth Nyamko, ilimtangaza pia Fadhili Mwanjegwa kuwa mshindi wa pili ambapo alijishindia zawadi ya pikipiki ya magurudumu matatu (Guta).

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, Meneja wa Kanda Assenga alisema kuwa kampeini hiyo inalenga kuhamasisha watanzania na wateja wa NMB kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba ili kuweza kukabiliana na dharura mbalimbali.

Alisema kuwa NMB inaamini kuwa watu wakijenga tabia ya kujiwekea kwenye akaunti zao wataweza kujiepusha na mikopo umiza, au kausha damu pindi wanapopata dharura inayohitaji fedha.

“ Tunawasisitiza zaidi wateja wetu wa NMB kujitokeza kwa wingi kushiriki kampeini hii ambayo inaendelea, wachangamkie fursa hii, watu wameshinda pesa taslimu, majiko ya umeme, trekta za kilimo, pikipiki, pamoja na TV janja,” alisema Assenga.

Alisema tangu kampeini hiyo imeanza jumla ya washindi 64 wamejishindia pesa taslimu, ambapo 60 kati ya hao wamejipatia kiasi cha Shilingi Laki moja (100,000) kila mmoja na washindi wanne wamejipatia Milioni tano kila mmoja.

Kwa upande wake Bernad Kimario mara baada ya kupatiwa zawadi ya trekta ya kilimo (Powertiller) alisema kuwa mwanzoni wakati anapigiwa simu kuwa ameshinda alihisi kuwa ni uongo au anataka kutapeliwa.

Alisema kuwa aliamua kwenda katika tawi la benki ya NMB kuulizia kama ni kweli, ndipo alipokutana na jina lake na kugundua kuwa Kampeini hiyo siyo uongo wala utapeli bali ni ukweli hivyo watu wajiwekee akiba ili waweze kushinda.

“ Nashukuru sana kwa nyenzo hii ambapo NMB imenipatia, sikutumia nguvu kubwa kuipata, ni kujiwekea akiba kwenye akaunti yangu, nawasisitiza watu washiriki, hii trekta itanisaidia sana kwenye kilimo changu cha mahindi na mchele,” alisema Kimario.

MWISHO.



Meneja Mauzo NMB Janeth Nyamko akiwa na Afisa wa Bodi ya michezo ya kubahatisha, wakiendesha droo ya 10 ya Kampeini ya Bonge la Mpango inayoendeshwa na Benki ya NMB, droo hiyo ilichezeshwa jana mjini Kahama Shinyanga.



Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم