Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
MKUU wa Mkoa wa Simiyu Kenan Kihongosi amestukia Wizi wa Mbegu za Pamba unaondelea kufanywa na baadhi ya Wafanyabiashara wakishirikiana na Viongozi wa vyama vya Ushirika (Amcos).
Akizungumza jana kwenye Kikao cha kujadili mifumo ya Masoko ya Mazao ya Nafaka na mazao mchanganyiko, kilichofanyika katika Ukumbi wa Bariadi Conference mjini Bariadi, Kihongosi alisema kuna Wizi Mkubwa sana wa mbegu za Pamba katika Mkoa huo.
Alisema tayari wameshakamata watu wakiwa na mbegu za Pamba zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kupelekwa mashambani kwa wakulima katika msimu wa Kilimo 2024/25 na badala yake zinauzwa ili kukamuliwa Mafuta licha ya kuwa na sumu.
"Ninapozungumza hapa, Kuna watu tumewakamata na Tani za kutosha za mbegu ya Pamba...Jana pia tumemkamata mtu akiwa na tani 20 za mbegu za Pamba na tulichokubaliana ni kwenda Mahakamani moja kwa moja na asiwepo wa kumtetea sababu tutamuunganisha" alisema Kihongosi.
Alieleza kuwa, haiwezekani serikali inatoa fedha ili kununua mbegu za Pamba lakini viongozi wa Amcos wanachukuw mbegu na kuzipeleka Mwanza kukamuliwa Mafuta huku wakulima wakiilalamika kutotosheleza.
Aliwataka viongozi wanaohusika na sekta ya Kilimo ikiwemo vyama vya Ushirika (Amcos) kubadi ili kuhudumia wakulima kama ambavyo serikali imejipanga na kwamba Biashara ya kuunguana na Viongozi wa Amcos itawamaliza.
Aonya Wafanyabiashara wanaokwamisha Wakulima.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa alowaonya Wafanyabiashara na Wanunuzi wa Mazao wanaokwamisha jitihada za Serikali katika kumkomboa mkulima.
Aidha alizitaka Mamlaka zote zilizopo chini ya Wizara ya Kilimo ndani ya Mkoa huo kujipanga ili kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kwamba asiwepo yoyote atakayehujumu sera za Serikali kwa kuchezea wanaochezea mifumo.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao, Irene Mlora alisema serikali imeunda chombo cha kusimamia mazao yasiyokuwa na Bodi ili kutimiza adhma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba wakulima wanufaika na jasho lao.
Alieleza kuwa serikali imejipanga kurasimisha minyororo ya thamani ili kuongeza bei ya mazazo, mkulima kwa wakati, kupata takwimu halisi za mazao na kurahisisha ukusanyaji wa mapato.
Alisema serikali itaweka mifumo wezeshi kwenye Amcos kupitia mifumo ya Ushirika na ukusanyaji mazao ili kumlinda mkulima na kwamba Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi ya Ghala itakuwa inatoa bei elekezi ya mazao ya nafaka kwenda kwa wakulima.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shemsa Mohammed alisema wanaunga mkono Ununuzi wa Mazao ya nafaka kupitia mfumo wa Stakabadhi ya Ghala sababu Ilani ya Uchaguzi imeelekeza.
Mwigulu Lubinza, mfanyabiashara wa Nafaka aliiomba serikali kuboresha mazingira ya mfumo huo ikiwemo utoaji wa vibali na leseni za maghala sababu zoezi la Ununuzi wa Nafaka limeshaanza ambapo baadhi ya Wafanyabiashara walikuwa wameshaanza kununua mazao ya nafaka kutoka kwa wakulima.
Mwisho.
Mbegu za Pamba.
إرسال تعليق