
CCM imemtaka Jussa kutozichezea akili za wazanzibari kwani maendeleo anayoyaponda yako sanjari na ahadi zilizomo katika Ilani ya Uchaguzi ya ACT mwaka 2020/2025.
Siri hiyo imefichuliwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis , aliyesema baadhi ya ahadi zilizotekelezwa na SMZ chini ya Rais Dkt. Huseein Mwinyi , zimo katika Ilani ya ACT Wazalendo .
Mbeto akionyesha kumshangaa Jussa ,amesema yalioahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2020- 2025, yanafanana na ahadi za ACT, hivyo ni kituko kumsikia Jussa akibeza ujenzi wa shule za Maghorofa.
Akitoa mfano , amesema katika kifungu cha 4.3 kuhusu Michezo, Sanaa na Burudani , ukurasa wa 39, ilani ya ACT, kama kingeingia ikulu , kiliahidi kuimarisha maeneo ya mapumziko kwa kushiriana na vikundi vya Wanawake na Vjana ili kuongeza ajira.
Pia Mbeto amekitaja kifungu cha 3.2.1 cha ilani ya ACT, imeahidi endapo kingeshinda uchaguzi , kingeboresha Miundombinu ya huduma za Afya kwa kujenga Zahanati ,Vituo vya Afya na kuzijengea uwezo hospitali za Wilaya na Mikoa.
"Nimewahi kusema mahali fulani Jussa kifikra na kiitikadi hana tofauti na kibaraka wa zamani huko Zimbabwe Ian Douglas Smith .Kazi yake kubwa ni kupinga mema yote ya kimaendeleo kwa Afrika na watu wake", ameeleza Mbeto.
Katibu huyo Mwenezi , amesema juhudi za kimkakati na kisera zilizofanywa na Serikali ya Rais Dk. Mwinyi kupitia ilani ya CCM mwaka 2020 - 2025, ametekeleza kwa ufanisi mkubwa sekta za Elimu, Uwekezaji, utalii Michezo ,Sanaa na Afya ,tena kwa kiwango cha juu.
"Jussa na ACT msiwafanye wananchi wa Zanzibar hawajui malengo yenu . Mmeshindwa kutekeleza mradi wenu wa siri acheni kuburuza wananchi .Rasilimali na Maliasili za Zanzibar zipo , zitawanufaisha wazanzibari si vinginevyo ",amesema Mbeto.
Kwa muktadha huo ,CCM imewataka wananchi wa Zanzibar na wafuasi wa ACT, kuamka na kuyatafakari maneno ya Jussa kila anapotamka kwani ameamua kuwa komedi wa kisiasa akiamini atawachekesha walionuna.
'Serikali ya awamu ya nane imejenga Viwanja vya soka vya kisasa , imeimarisha studio za Sanaa na Wasanii. Zimejengwa Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo vya Amali ,Zahanati , hospitali za wilaya na Mikoa", amesema Mbeto.
Mbeto amemtaka Jussa kama kweli yeye si kibaraka ,ajitokeze akanushe kama ACT haikuahidi ahadi hizo.
Amesema CCM kupitia ilani yake ya uchaguzi mwaka 2020 hadi 2025 chini ya serikali ya Rais Dkt. Mwinyi imetimiza wajibu wake .
"Wana ACT wasidanganywe na Ian Smith . Waisome ilani yao ya uchaguzi mwaka 2020 -2030 waone kama yaliotekelezwa na SMZ kama si yale yaliomo kwenye ilani yao . Jussa si kibaraka tu ni kiongozi mawenge", amesisitiza Mbeto
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق