TANZANIA YAZUNGUMZIA UMUHIMU WA USIMAMIZI BONDE LA MTO NILE.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew (katikati) akiwa kwenye Mkutano wa nchi Mwanachama wa Blonde la Mto Nile, uliofanyika Addis Ababa-Ethiopia.


 Addis Ababa- Ethiopia. 


NCHI ya Tanzania imezitaka jamii za nchi Wanachama wa Bonde la Mto Nile kuungana kwa pamoja ili kuhakikisha usimamizi bora wa Rasilimali za Maji katika Bonde hilo, ambao hutegemewa na watu zaidi ya milioni 270 katika ukanda huo.


Akizungumza kwenye Mkutano wa nchi Mwanachama uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia, Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew amezungumzia umuhimu wa maji kama chanzo kikuu cha kiuchumi na kiusalama wa chakula, na kusema kuwa ushirikiano wa pamoja ni muhimu ili kuhakikisha kuwa maji ya Mto Nile yanatumika kwa usawa kwa nchi zote katika bonde hilo.


“Tuna jukumu la kuhakikisha kwamba usimamizi wa Bonde la Mto Nile unafanyika kwa njia ya usawa na kwa manufaa ya wote...Maji ni rasilimali ya muhimu kwa watu wa Bonde la Mto Nile, na tunahitaji kufanya kazi kwa pamoja ili kuyaendeleza na kuyatumia vyema,” amesema Mhandisi Kundo


Kundo amesisitiza kuwa ushirikiano thabiti unahitajika ili kudumisha amani na maendeleo ya jamii zinazotegemea mto huo.


Amesema kuwa Tanzania inataka kuona Mataifa yote yanahusishwa kikamilifu katika mchakato wa usimamizi na maendeleo ya Bonde la Mto Nile, kwa manufaa ya wananchi wake.


Mhandisi Kundo amesema Serikali ya Tanzania imeona umuhimu kwa nchi wanachama wa Bonde la Mto Nile kuonyesha uwazi, uwajibikaji, na ushirikiano kwa maslahi ya pamoja, huku wakizingatia umuhimu wa uongozi bora na matumizi sawa ya rasilimali hiyo ya maji


Mto Nile ni chanzo kikuu cha maji kwa nchi za Sudan, Ethiopia, Misri, Uganda, Rwanda, Kenya, Tanzania, na Burundi na kwamba Maji yake hutumika kwa kilimo, uzalishaji umeme, usambazaji wa maji, na shughuli nyingine za maendeleo, na hivyo ushirikiano wa nchi hizi ni muhimu kwa kuhakikisha usalama wa maji na maendeleo endelevu.


Mwisho.



Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew (katikati) akiwa kwenye Mkutano wa nchi Mwanachama wa Blonde la Mto Nile, uliofanyika Addis Ababa-Ethiopia.




Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم