Na Mwandishi wetu. Simiyu.
FISI mmoja ameuwawa katika kijiji cha kimali kata ya Nyamalapa wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu na kikosi cha askari wa Mamlaka ya Wanyamapori nchini, (TAWA), Tanapa na jeshi la polisi wilayani humo ,huku mnyama huyo amekutwa akiwa na alama ya jina upande wa paja lake la kushoto na shanha shingoni.
Mkuu wa wilaya ya Itilima Anna Gidarya akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamigagani kata ya Mwalushu amewataka wananchi wote wilayani humo , wanaomiliki nyara za serikali kinyume na sheria za wanyamapori kuzisalimisha haraka iwezekanavyo kwa wahusika wa uhifadhi kabla ya hatua kali hazijachukuliwa dhidi yao.
Kumekuwepo na matukio ya fisi kushambulia watoto kuanzua majira ya ya saa moja usiku katika maeneo tofauti tofauti wilaya ya itilima ambapo mpaka sasa fisi 16 wameuwawa na kikosi kazi cha askari wa TAWA ,TANAPA na jeshi la polisi wilaya ya itilima
Mwisho.
إرسال تعليق