Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Iddi Kiyogomo akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani).
Na Fadhili Abdallah, Kigoma.
JESHI la Polisi Mkoani Kigoma limewaua kwa kuwapiga risasi watu watatu wanaotuhumiwa kuwa majambazi wakituhumiwa kutaka kuhusika kwenye tukio la utekaji kwa kutumia silaha ambapo pamoja na vifo hivyo pia bunduki mbili za kivita zimekamatwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma, Iddi Kiyogomo akitoa taarifa kwa waandishi wa habari alisema kuwa tukio hilo limetokea majira ya jioni Februari 20 mwaka huu katika kijiji cha Heru shingo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Kamanda Kiyogomo alisema kuwa awali polisi wa doria wakiwa kwenye majukumu yao waliapta taarifa ya kuwepo kwa watu wenye nia ya kufanya uhalifu hivyo wakaweka mtego ili kuwatia nguvu na ndipo yakatokea mapigano ya kurushiana risasi na watu watatu wakauawa katika tukio hilo.
Alisema Kaimu kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma kuwa sambamba na vifo vyaa watu hao watatu ambao miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Kasulu pia bunduki mbili za kivita aina ya AK – 47 zikiwa na magazine mbili na risasi 52, mapanga mawili na marungu mawili vilikamatwa.
Hadi sasa polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kujua kama marehemu au walikuwa watanzania au raia wa kigeni ambapo watu wengine ambao idadi yao haijajaulikana walikimbia na polisi inaendelea na msoko na kwamba hali ya Amani imedhibitiwa.
Mwisho.
إرسال تعليق