Theresia Noel akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shule ya elimu (DUCE).
Na Mwandishi wetu.
MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umepongezwa kwa kufanikisha kutimiza ndoto ya Mwanafunzi wa mwaka wa pili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shule ya Elimu (DUCE), Theresia Noel ambaye ni mlemavu wa viungo, kwa kuwa mnufaika kuanzia shule ya Msingi hadi ngazi ya Elimu ya juu.
Awali Akizungumza na Waandishi wa habari, Theresia ameshukuru TASAF ilivyochangia kufanikisha ndoto zake hizo katika elimu na pia kumshukuru na kumuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuendelea kutunisha mfuko huo ili uweze kusaidia Watanzania masikini waweze kujikwamua.
Kwa upande wake, Bibi Angelina ambaye ni mlezi wa Theresia mnufaika wa TASAF akizungumza na waandishi wa habari, amesema amemlea mjukumu wake huyo baada ya kutelekezwa na mama yake akiwa na miezi sita.
Ambapo aliweza kumlea na kupata elimu shule ya Msingi Jeshi la Wokovu, na kisha aliendelea na Sekondari shule ya Wasichana Jangwani, na sasa mwaka wa pili katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Shule ya Elimu (DUCE).
Mwisho.
إرسال تعليق