WIZARA ZA KILIMO, UJENZI, VIWANDA NA BIASHARA KUSHIRIKIANA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA NJOMBE.

 



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


BAADHI ya Wafanyabiashara Mkoani Njombe wameitaka serikali kupunguza matuta ya barabarani pamoja na vituo vya ukaguzi ambavyo vimekuwa kikwazo kikubwa katika biashara zao.


Wameyasema hayo mbele ya Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Jafo, Wafanyabiashara hao akiwemo Zacharia Chaula Benadetha Sanga, Mhema Oraph na Eloy Mbilinyi, wameeleza kuwa wingi wa matuta barabarani yanapoteza muda mwingi katika kusafirisha mizigo pamoja na vituo vya ukaguzi ambavyo vimekuwa vikichelewesha shughuli za kibiashara.


Wengine wamesema vituo vingi vya ukaguzi wa  Magari watendaji wake Wamekuwa kikwazo kwani wanaendekeza Rushwa kupitisha Magari ya mizigo jambo ambalo linakatisha Tamaa ya kuendelea na biashara.


Awali Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema baadhi ya changamoto zikiwemo za kwenye vituo vya ukaguzi alielekeza kupunguza vikwazo kwenye baadhi ya mizigo hasa mazao ya kuoza ili kunusuru hasara anayoweza kupata mfanyabiashara na Serikali yenyewe.


Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa Njombe Siphael Msigala amesisitiza suala la kupunguza Mlundikano wa Kodi kwenye biashara Moja ili kuondoka malalamiko ya miaka mingi.


Akijibu Hoja za wafanyabiashara mbalimbali Waziri wa viwanda na biashara Dkt. Seleman Jafo amesema Wizara yake inaendelea kushughulikia changamoto hizo huku akiahidi kwenda kushirikisha Wizara nyingine katika kuweka Biashara katika mstaari Mnyoofu.



Mwisho.

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم