Na Gabriel Kilamlya, Habari na Matukio APP NJOMBE
RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewashika mkono watoto 335 wa vituo 10 vya watoto Yatima na walemavu katika mkoa wa Njombe kwa kuwapa misaada mbalimbali ya vyakula kwa ajili ya kusherekea siku kuu ya Eid El Fitir.
Akikabidhi baadhi ya misaada hiyo katika kituo Cha watoto Yatima na walemavu Cha Renato Grand Ilembula kwa niaba ya Mkuu wa Njombe wa Njombe Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Zakaria Mwansasu amesema pamoja na misaada hiyo lakini jamii inapaswa kuwajali watoto na kujiepusha na ndoa za utotoni na kuingia kwenye mahusiani pasina maandalizi.
Tarcisio Moreschi ni Paroko wa parokia ya Ilembula ambaye anasema kituo hicho chenye watoto 90 hivi sasa licha ya kuwa na Maendeleo Mazuri lakini watoto wanakosa Upendo toka kwa baadhi ya wazazi na walezi ambao hawafiki kuwaona.
Tumwombe Kidumba na Jestina Sapali wameshukuru kwa misaada hiyo toka kwa Rais Samia na kwamba itawasogeza katika siku
Subilaga Mwaigwisya Ofisa ustawi wa Jamii mkoa wa Njombe ambaye anasema wamepeleka Mchele,Sabuni,Unga wa ngano,Mafuta na soda kwa ajili ya Watoto hao na kwamba Jamii inatakiwa kuendelea kuwasaidia katika maeneo yao kupitia vituo vilivyopo karibu.
Mwisho.
Post a Comment