MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Steven Wasira (katikati), kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Shemsa Mohammed, kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Maswa Onesmo Makota.
Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Steven Wasira amewasili katika wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu kwa ajili ya ziara ya kikazi kwa muda wa siku tatu.
Akiwa Mkoani Simiyu, Wasira atafanya vikao vya ndani na mikutano ya hadhara katika wilaya za Meatu, Itilima, Bariadi na Busega.
Makamu Mwenyekiti (Wasira), pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Simiyu.
Mwisho.
Post a Comment