WATOTO WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KWA KUZAMA KWENYE SHIMO LA MAJI




Na Mwandishi wetu.


WATOTO wawili wa familia moja, katika kitongoji Ihula kijiji cha Bulumbaka kata Mwaubingi, Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, wamefariki kwa kudumbukia kwenye shimo la maji yanayosadikiwa kuwa na kemikali za kuchenjua dhahabu kwenye mgodi wa Gasuma namba moja uliopo kijijini hapo.


Kaimu kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Simiyu, ASF Faustin Mtitu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akitaja chanzo kuwa ni kunywa maji hayo na kukosa hewa ya oksijeni.

Kamanda Mtitu, amewataja watoto hao wa familia moja kuwa ni Yona Chai (7) na Baraka Balida (3).

Mwisho.





Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post