Na Costantine Mathias, Meatu.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu kimesema kuwa kimeridhishwa na Utekezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika sekta za Afya, Elimu, Maji, Umeme, Barabara na miundombinu mingine huku kikiwapongeza watumishi wa serikali katika Usimamizi wake.
Aidha, CCCM imeitaka serikali kuhakikisha wanakamilisha miradi inayojengwa ikiwemo vyumba vya madarasa, zahanati, miradi ya Maji, ambayo imefikia katika hatua mbalimbali za ujenzi ili iweze kukamilika kwa wakati na kuanza kutumika.
Hayo yamebainishwa juzi na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa huo, kwenye kikao kilichofanyika wilayani Meatu kwa ajili ya kujadili taarifa za Utekezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 huku wakimpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kutekeleza miradi ya Maendeleo.
Awali Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Faudhia Ngatumbura amesema wanasimamia miradi ya Maendeleo ili kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma Kwa wananchi.
"Tumeendela kusimamia miradi ya Maendeleo ili kuhakikisha serikali inaboresha utoaji wa huduma, ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Viktoria upo katika hatua nzuri kwa sababu ujenzi wa Matenki unaendelea, kituo cha kupozea Umeme kinaendelea kujengwa na hii ni baadhi ya miradi mikubwa katika Mkoa wetu na ikikamilika itatatua changamoto ya Maji na Umeme" amesema Faudhia.
Katibu wa CCM Mkoa huo, Eva Ndegeleki amesema wamepita kila wilaya kukagua ujenzi wa miradi ya Maendeleo na kubaini kuwa Miradi hiyo imejengwa vizuri na umeshaanza kutumika ikiwemo miradi ya Maji, Elimu, na Majengo ya kutolea huduma za Afya.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MNEC), Gungu Silanga amewapongeza watumishi hao kwa Usimamizi mzuri wa miradi ambayo imeonyesha viwango na Ubora huku akiwasisitiza kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali ili serikali ya CCM iendeleee kuwa madarakani.
Kabla ya kufanyika kikao hicho, Kamati ya Siasa ilifanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo katika wilaya za Busega, Bariadi, Itilima, Maswa na Meatu.
Mwisho.
Post a Comment