MrJazsohanisharma

KADI 27,123 ZA KIELEKTRONIKI ZA CCM KUSAMBAZWA SIMIYU.

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu, Lumeni Mathias akionyesha kadi mpya ya CCM ya kielektroniki iliyoboreshwa.


Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu, Lumeni Mathias amewataka Wana-CCM mkoani humo, kwenda kuchukua kadi zao za kielektroniki kwenye Ofisi za Makatibu wa CCM wa Matawi ili wawe na sifa za Uanachama pamoja na kushiriki Matukio muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu.



Amesema kuwa kadi hizo mpya zimeboreshwa zaidi tofauti na kadi za zamani ambazo hazikuwa na baadhi ya taarifa ikiwemo kuonyesha Mkoa, wilaya, kata na tawi analotokea Mwanachama.


Lumeni, ameyabainishwa leo, April 2, 2025, wakati akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake na kueleza kuwa kadi 27,123 zitasambazwa Mkoani Simiyu.


"Kadi zetu za kielektroniki zimekuja, Mkoa wetu wa Simiyu tumepata kadi 27,123  kwa ajili ya Wana CCM waliojiandikisha kwenye mfumo wa kielektroniki...kila Mwanachama aliyejiandikisha aende kwa Katibu wa CCM wa Tawi lake aweze kupata kadi yake mpya na iliyoboreshwa" amesema Lumeni.


Ameeleza kuwa, kadi hizo zimeboreshwa kwa hali ya juu sana, ambapo huko nyuma walianza kupata kadi za aina hiyo lakini zinazotolewa sasa zimeboreshwa zaidi.


Lumeni amefafanua kuwa kadi hizo zinatolewa bure ambapo Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan ameamua kutoa kadi hizo bure.


Amewataka wanachama watakaopata Kadi hizo kulipa ada ya Uanachama wao kupitia namba ya malipo (control number) iliyopo kwenye Kadi hiyo ambapo mwaka mmoja ni Tsh. 1,200/=.


"Kadi hizi ni muhimu sababu inamtambulisha Mwanachama wa CCM, pia inawapa uhalali wa kuomba nafasi ya Uongozi ndani ya CCM hususani kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025...lazima utajaza namba ya kitambulisho chako pia uwe Mwanachama halali ambaye unalipa ada, tutumie fursa hii kwenda kuchukua fomu kwa Makatibu wa Matawi" amesema.


Mwisho.

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu, Lumeni Mathias akionyesha kadi mpya ya CCM ya kielektroniki iliyoboreshwa.


KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu, Lumeni Mathias akiwaonyesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kadi ya CCM ya kielektroniki ya zamani.





Kadi Mpya ya CCM ya kielektroniki iliyoboreshwa.



Kadi ya zamani ya kielektroniki ya CCM.







Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post