
UJENZI wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria unaendelea kutelekezwa Mkoani Simiyu kwa gharama ya shilingi Bil. 440 umefikia hatua mbalimbali ambapo katika wilaya ya Itilima, Mradi huo umefikia asilimia 23.
Wajumbe wa Kamati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Simiyu, wametembelea ujenzi huo katika wilaya ya Itilima na kukagua ujenzi wa Tanki lenye ujazo wa lita Mil. 10.
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), wilaya ya Itilima, Mhandisi Yahaya Hussein amesema baada ya Mradi huo kukamilika itahudumia vijiji 28 na itaongeza upatikanaji wa Maji katika wilaya hiyo kufikia asilimia 95.
"Mradi huu utaruhusu kufanya upanuzi kwenda vijij vingine na pia Tanki kitaruhusu kupeleka Maji wilaya ya Itilima... Mradi huu utafikia wakazi 300,000, Tunamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za kutekeleza miradi ya Maji." Amesema Mhandisi Hussein.
Diwani wa Kata ya Chinamili, Nindwa Bukanu amemshukuru Dk. Samia kwa kazi ya kuwaletea Maji na Wananchi wa kata ya chinamili.
Ameeleza kuwa awali walikuwa na shida ya kupata Maji safi na salama, lakini sasa wanaenda kupata Maji ya uhakika.
Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Eva Ndegeleki amesema Maji ni moja ya vitu endelevu katika Ilani ya CCM ambapo serikali imeweka mkazo ili kuhakikisha wananchi wanapata Maji safi na salama.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenan Kihongosi amesema kukamilika kwa Mradi huo kutatua kero ya Maji katika Mkoa huo huku akiwataka wananchi kuendelea kuunga Mkono jitihada za serikali pamoja na kulinza amani.
Amesema ujenzi wa Tanki la lita mil. 10 katika wilaya la Itilima litarahisisha kusambaza Maji katika vijiji 28 vya Itilima.
"Mradi huu uaanzia Busega kuja Bariadi na Itilima, baadae Meatu na Maswa,
Wajibu wetu ni kusimamia Mradi...tunaomba wakandarasi waongeze kazi, thamani ya fedha na Ubora wa Mradi vinaonekana na tumeona vijana wanaozunguka maeneo haya wameajiriwa" amesema Kihongosi.
Mwisho.





Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق