Tanki la Maji lenye ujazo wa lita 100,000 linalojengwa katika Kijiji cha Mwashata wilayani Meatu 

Na COSTANTINE MATHIAS, Meatu.


WANANCHI zaidi ya 14,000 wa Vijiji vya Mwabuma, Mwashata na Baluli wilayani Meatu Mkoani Simiyu wameanza kunufaika na Mradi wa Maji uliyojengwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa gharama ya shilingi Bil.10.9.


Akitoa taarifa ya Ujenzi wa Mradi huo mbele ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inayokagua Utekelezaji wa Ilani, Kaimu Meneja wa RUWASA, Mhandisi Bruno Paul amesema Mradi huo umekilika kwa asilimia 98 na kwamba Mkandarasi ameshalipwa zaidi ya shilingi Mil. 700.


Ameeleza kuwa katika mradi huo, wamejenga vituo 8 vya kuchotea Maji, birika la kuchotea Maji pamoja na Tanki lenye ujazo wa lita 100,000.


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Gungu Silanga amesema, wanalapita kukagua Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo kama walivyoahidi kupitia Ilani ya Uchaguzi.


"Tumekagua Mradi ni mzuri na wananchi wameanza kupata Maji safi na salama...
Tutaiomba Wizara ya Maji, kuleta fedha ili kukamilisha ujenzi wa Mradi wa Maji huu" amesema Gungu.


Mwisho.




Chanzo Cha Mradi wa Maji Mwashata kilichojengwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).


Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM, Mkoa wa Simiyu wakiangalia koki kwenye Mradi wa Maji Mwabuma.