MWAUBINGI WAMCHANGIA ENG. KUNDO FEDHA ZA KUCHUKUA FOMU YA UBUNGE.





Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.



WANACHAMA wa Chama Cha Mapiduzi (CCM), kata ya Mwaubingi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu wamechanga na kukabidhi fedha kiasi cha Shilingi 900,000/= kwa ajili ya kumchukulia fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Bariadi Vijijini, Mhandisi Kundo Mathew. 

Wanachama hao wamesema kuwa wameridhishwa na utendaji kazi wa Mbunge huyo wa Jimbo la Bariadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji kwa kutekeleza kisawasawa Ilani ya CCM 2020/2025 katika sekta mbalimbali za miradi ya maendeleo. 

Wakizungumza kwenye mkutano maalumu wa kuwasilisha Utekelezaji wa Ilani ya CCM, uliofanyika katika shule ya sekondari Gasuma, wamesema kuwa wanampongeza Rais Dk. Samia Sulubu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza. Miradi ya maendeleo kwenye miradi ya Maji, Elimu, Umeme, Barabara na mawasiliano akishirikiana na Mbunge wa Jimbo hilo.

Katika hatua nyingine, Wanachama hao pia wamechangia Diwani wa Kata hiyo, Richard Buyamba kiasi cha shilingi 100,000/= kwa ajili ya kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Udiwani.


Katibu Kata wa Kata ya Banemhi, Siasa Ndege amesema wanachama hao wameridhishwa ma Utekelezaji wa Ilani ya CCM na kwamba kwa nia Moja wanachama hao wamechangishana fedha hizo na kumkabidhi Mhandisi Kundo ili achukue fomu kugombea Ubunge kwenye uchaguzi Mkuu utaokaofanyika Oktoba 2025.

Akipokea fedha hizo, Mbunge huyo amewashukuru wanachama hao na kuwaahidi kuendelea kuwatumikia kwa nia ma moyo mmoja.











Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post