MBUNGE wa Jimbo la Bariadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew akiongea na wanachama wa CCM kata ya Mwaubingi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MBUNGE wa Jimbo la Bariadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew amewasilisha Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025 katika kata ya Mwaubingi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu ambapo katika miaka mitano wananchi wamenufaika na miradi ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bil. 1.2.
Akizungumza na wajumbe wa Mkutano maalumu wa kata ya Mwaubingi, Mhandisi Kundo amesema uwasilishaji wa Ilani hiyo ni Kuweka msisitizo juu ya miradi iliyotekelezwa na serikali ya Dk. Samia Suluhu Hassan.
"katika miaka mitano toka 2015 hadi 2020 kata hii ilipata fedha za miradi ya maendeleo kiasi cha Mil. 297, lakini kwa miaka mitano ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, serikali imetekeleza miradi ya shilingi Bil. 1.2 kwenye sekta za Umeme, Elimu, Afya, Maji, Barabara na Madaraja ambayo ni hatua kubwa sana kimaendeleo" amesema Mhandisi Kundo.
Mhandisi Kundo ameongeza kuwa agenda za maendeleo zinatoka kwa wananchi ambapo viongozi hao wakiwemo Madiwani, Wabunge na Rais wanawatumikia wananchi kulingana na mahitaji yao huku akisisitiza kuwa Uwakilishi ni kusema agenda za wananchi.
Katika hatua nyingine, Mbunge huyo amekabidhi mipira minne na pea moja ya jezi kwa kila Kijiji katika vijiji vya Gasuma, Mwaubingi na Bulumbaka wakati huo kata ya Mwaubingi ikikabidhiwa jezi pea Moja na mipira mitatu pamoja na pampu Moja ya maji kwa Kila Kijiji.
Awali Diwani wa Kata ya Mwaubingi, Buyamba kiberiti amesema kuwa wamepata mradi wa wenye thamani ya shilingi Mil. 600 ambao umekamilika na kila Kijiji wanapata maji.
Amesema anaipongeza serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za miradi ya umeme, ujenzi wa barabara na madaraja ambayo yamerahisisha shughuli za uchumi.
Mwisho.









Post a Comment