Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
CHAMA cha Wanunuzi wa Pamba nchini (TCA), kimesema kuwa kitanunua pamba yote iliyozalishwa na wakulima katika msimu wa kilimo 2024/2025.
Aidha, chama hicho kimeishukuru serikali kwa kuimarisha kilimo cha zao hilo pamoja na kutengeneza mazingira rafiki ambayo yameleta tija kwa wakulima.
Akizungumza na waandishinws Habari, Katibu wa TCA, Boaz Ogolla amesema wanunuzi wa pamba wamejipanga sawasawa kununua pamba yote itakayozalishwa na wakulima baada ya serikali kuongeza ufuatiliaji kwa lengo la kupata pamba yenye ubora.
Ogolla ambaye pia ni Meneja wa Kampuni ya kuchambua pamba ya Alliance Ginneries, ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha huduma za ugani kwa wakulima hao imeongeza mavuno ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Amesema, wanunuzi wa Pamba wako tayari kununua pamba yote na kwamba maandalizi kwa ajili ya misimu wa ununuzi 2025 yamekamilika na kamba wanatarajia uzaliashaji itaongezeka.
"Tumejiandaa kununua pamba yote, lakini ukiangalia kama uzalishaji umeongezeka... Na hii inatokana na jitihada za serikali kuanzisha mpango wa BBT ambayo imechangia kwa sehemu kubwa".amesema Ogolla.
Ogolla ameishukuru Bodi ya Pamba Tanzania kwa kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo kwa wakati na pia ufutiliaji wa wakulima mashambani.
Mwisho.

Post a Comment