Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa kata ya Banemhi kwa ajili ya kuwasilisha Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025.Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
WANANCHI wa Kata ha Banemhi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu wameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza miradi ya Maendeleo ikiwemo kukamilisha ujenzi wa daraja la Mwadobana ambalo lilikuwa kikwazo cha Maendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya Wananchi hao, Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew amesema kuwa serikali ya Rais Dk. Samia imeendelea kuimarisha na kuboresha huduma za kijamii ikiwemo Elimu, Afya, Umeme na Barabara ambazo zimeimarisha uchumi na kiwaongezea vipato.
"Toka Uhuru, Jimbo la Bariadi tulikuwa na madaraja 38...lakini ndani ya Miaka mitano ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan tumejenga madaraja 45 likiwemo daraja la Mwadobana ambalo lilikuwa kikwazo cha maendeleo lakini pia imetekelezwa miradi yenye thamani ya shilingi Bil. 1.8 katika kata hii" amesema Mhandisi Kundo.
Amesema wanamshukuru Rais Dk. Samia kwa kutekeleza Ilani ya CCM ambayo imesimamiwa na serikali kupitia watendaji huku akiwasisitiza kuchagua viongozi wanaotokana na CCM katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu ili waendelee kuwahudumia.
Pamoja na kuwasilisha Ilani ya CCM, Mbunge huyo pia amekabidhi mipira 23 na jezi pea sita ambapo Kijiji cha Mbugani, Banemhi, Kilabela, Mwaunkwaya na Nsanzaguma Kila kimoja kimepata mipira minne na pea Moja ya jezi huku kata ya Banemhi ikikabidhiwa mipira mitatu na pea Moja ya jezi pamoja na pampu za maji.
Mwisho.







Post a Comment