CCM SAKWE WAMKABIDHI CHETI CHA PONGEZI, ENG. KUNDO.

MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew (kulia) akipokea cheti cha Pongezi toka kwa viongozi wa kata ya Sakwe baada ya Kutambua mchango wake kimaendeleo.


Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


CHAMA cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Sakwe wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, kimemkabidhi cheti cha Pongezi Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew kutokana na utendaji wake mzuri ndani ya miaka mitano.


Akikabidhi kwa niaba ya Wanachama, Katibu wa CCM kata hiyo, Mrema Isungi amesema ahadi alizotoa Mbunge huyo, Mhandisi Kundo wakati anaomba kura (2020), amezitimiza. 


"Tunakukabidhi cheti hiki cha pongezi kwa kutambua mchango wako kwenye maendeleo, umetimiza ahadi za kutuletea maendeleo kwa kushirikiana na Rais Dk. Samia ulizozitoa wakati unagombea...umeme, mawasiliano na maji yametufikia, tunakupongeza sana" amesema Katibu huyo. 


Katika hatua nyingine, Katibu huyo alimpongeza Rais Dk. Samia kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya maendeleo huku akiahidi kuwa watahakikisha wanampa kura za kishindo katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2025.


Akizungumza mara baada ya kupokea cheti hicho kwenye mkutano wa kuwasilisha Ilani ya CCM, Mhandisi Kundo amewashukuru wananchi, viongozi wa dini, watumishi wa umma pamoja na Wana CCM kwa ushirikiano wao katika kipindi cha miaka mitano akiwa Mbunge wa Jimbo la Bariadi. 


Mhandisi Kundo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, amesema uwasilishaji wa Ilani ya CCM (2020/2025) ni Kuweka msisitizo juu ya miradi iliyotekelezwa na serikali ya Dk. Samia  Suluhu Hassan.


Mhandisi Kundo ameongeza kuwa agenda za maendeleo zinatoka kwa wananchi ambapo viongozi hao wakiwemo Madiwani, Wabunge na Rais wanawatumikia wananchi kulingana na mahitaji yao huku akisisitiza kuwa Uwakilishi ni kusema agenda za wananchi. 


MWISHO.











Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post