ENG. KUNDO AGAWA JEZI, MIPIRA KATA ZA MWASUBUYA NA KILALO.

MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew akiangalia Moja ya mipira aliyoigawa kwenye kata za Mwasubuya na Kilalo.


Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew, ameendelea na ziara yake ya kutembelea Kata kwa Kata kwa lengo la kuwasilisha Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025.


Akiwa kata za Kilalo na Mwasubuya, Mbunge huyo ametoa wa msaada wa vifaa vya michezo zikiwemo jezi na mipira ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya michezo. 


Katika Kata ya Kilalo, kwenye vijiji vya Ikingulyambesi A, Ikingulyambesi B, Nyamisagusa, Kilalo Mashariki na Kilalo Kati alikabidhi mipira 23 na pea sita za jezi ili kuhamasisha michezo na kuendeleza vipaji vya vijana, ambapo kila Kijiji aligawa mipira 4 na jezi pea 1, huku kata ikikabidhiwa mipira mitatu na pea 1 ya jezi.


Katika Kata ya Mwasubuya, yenye vijiji vya Mwasubuya, Isengwa, Igabulilo na Miswaki, aligawa mipira 19 ya miguu na jezi pea 5 ambapo kila Kijiji kimepata mipira minne na jezi pea 1 huku kata ikipatiwa mipira mitatu na pea Moja ya jezi.


Mwisho. 












Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post