Mtanzania anayeishi Uingereza, Abdallah Nyaligwa, leo Juni 30,2025 amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Ubunge wa Jimbo Jipya la Itwangi, ambalo limegawanywa kutoka Jimbo la Solwa.
Nyaligwa mzaliwa wa Itwangi kutoka familia ya Chief Kaswende Shikira anakuja kuwania nafasi hii akiwa na kumbukumbu ya heshima na urithi wa familia yake, kwani ni mjukuu wa marehemu Chief Abdalla Fundikira, kiongozi mashuhuri na shujaa wa siasa, ambaye alijitolea kwa ustawi wa jamii na taifa.

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
Post a Comment