RUHORO ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA NGARA 2025-2030

    



Mbunge wa jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruhoro amechukua fomu ya maombi ya kugombea tena nafasi ya ubunge kwa kipindi kingine cha 2025/30 kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Fomu hiyo ameichukua leo Juni 30 2025 katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM Ngara Mkoani Kagera. 

 Hata hivyo vyombo vya habari vilivyokuwepo katika eneo la tukio walipotaka mahojiano hakuwa tayari kuzungumzia chochote zaidi alisema wakati ukifika atazungumza.

Ikumbukwe kuwa Mheshimiwa Ruhoro ni miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa  kwa wananchi wa jimbo lake kwani wananchi hao wamekuwa wakimchangia fedha kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea tena katika kipindi kingine 2025-2030.

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post