RAIS SAMIA AIPONGEZA MASWA.

-Aitaka kuchangamkia fursa ya SGR na Viwanda

Na Samwel Mwanga, Maswa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kasi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani na mwenendo mzuri wa ulipaji kodi, akisema ni kiashiria thabiti cha utendaji mzuri wa uongozi wa halmashauri hiyo.

Akihutubia maelfu ya wananchi Jumatano Juni 18, 2025 katika Uwanja wa Jamhuri, Nguzo Nane, wilayani Maswa, Rais Samia amesema kuwa 

i halmashauri inajitambua.

 kupata zaidi ya asilimia 96 ya lengo la mapato kabla ya mwaka kwisha si jambo dogo.

" Inaonyesha mpo makini, lakini bado mnaweza kufanya zaidi.”amesema.

Kwa mujibu wa taarifa aliyopewa, halmashauri hiyo ilikuwa imepangiwa kukusanya Sh3.6 bilioni kwa mwaka wa fedha 2024/25, na hadi kufikia Mei 2025 tayari ilikuwa imeshakusanya Sh3.46 bilioni, sawa na asilimia 96.2.

Fursa ya Reli ya SGR: “Msizikose”

Katika hatua nyingine, Rais Samia ameihimiza halmashauri hiyo pamoja na wananchi wa Maswa kuchangamkia fursa za ajira, biashara na usafirishaji zitokanazo na mradi wa reli ya kisasa ya SGR kipande cha Mwanza-Isaka, ambapo Wilaya ya Maswa itanufaika kwa kuwa na kituo maalum cha kushushia na kupakia mizigo katika eneo la Malampaka.

“Kutakuwa na ajira, zabuni na fursa nyingi wakati na baada ya ujenzi. Tujielekeze kwenye uzalishaji wenye kuongeza thamani, ili tukamilishe mnyororo wa thamani kwa kutumia usafiri nafuu wa SGR,” alisisitiza Rais Samia.

Viwekezaji wa Pamba Wapewa Baraka

Akiwa Maswa, Rais Samia amezindua kiwanda cha kuchambua pamba mbegu cha Shree Rajendra Agro Industry chenye thamani ya Sh12.4 bilioni na uwezo wa kuchakata hadi tani 350 kwa siku. 

Amesema kiwanda hicho kitatoa ajira kwa wananchi, kuongeza thamani ya pamba, na kuleta uhakika wa soko kwa wakulima wa eneo hilo.

“Pamba yote ya Maswa itanunuliwa na kiwanda hiki. Hii itahakikisha mkulima anapata bei nzuri inayosimamiwa na Serikali. Niwaombe waendelee kulima kwa bidii, kwa sababu soko na viwanda vipo,” amesema.

Kwa msimu wa kilimo 2024/25, Rais Samia alisema mkoa wa Simiyu unatarajia kuzalisha tani 278,354 za pamba mbegu, huku Maswa pekee ikikadiriwa kuvuna tani 60,438.

Kiwanda cha Chaki: Serikali yaongeza moyo

Katika hatua nyingine, Rais Samia ameagiza Halmashauri ya Maswa kutenga eneo jingine kwa ajili ya malighafi ya kiwanda cha chaki cha wilaya hiyo, akisisitiza kuwa uzalishaji wa chaki ni wa kimkakati kwa taifa, na kinatakiwa kuwa na upatikanaji wa uhakika wa rasilimali.

“Hatuwezi kuwa na kiwanda bila uhakika wa malighafi. Tengeni eneo la kuchimbia malighafi ili chaki isizuiwe na changamoto ya upatikanaji wa malighafi,” amesema.

Rais Samia yupo mkoani Simiyu kwa ziara ya siku tano inayojumuisha kukagua, kuzindua, na kuweka mawe ya msingi ya miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza maoni na kero za wananchi.

Mwisho fursa ya SGR na Viwanda

Na Samwel Mwanga,Maswa.

Mwisho. 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post