NA COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MBUNGE wa Jimbo la Baruadi, Mhandisi Kundo Mathew amewasilisha Utekelezaji wa Ilani katika kata ya Mhango na kueleza kuwa serikali imetekeleza miradi ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Bil.6.4 ndani ya miaka mitano.
Mhandisi Kundo amesema kuwa serikali ya Rais Dkt. Samia imetekeleza miradi ya Maendeleo huku akiwataka wananchi kuendelea kuiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ikifika mwezi Oktoba wamchague Rais Samia pamoja na viongozi wengine wa CCM
"Tulikabidhiwa Ilani ya CCM, leo tumekuja kuwapa taarifa tulichokifanya Kwa miaka mitano...Kata hii imepokea shilingi Bil. 6.4 ambazo zimetolewa kwenye kata hii Kwa ajili ya miradi ya Maendeleo" amesema Mhandisi Kundo.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo ametoa Mipira 41 na jezi pea 9 kwenye Mitaa minane ya kata hiyo ambapo kila kata imepata mipira mitatu na jezi pea moja huku kata ikikabidhiwa mipira mitatu na pea moja ya jezi ili kuendeleza sekta ya michezo
.
Mwisho.









إرسال تعليق