
Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amewaka Wananchi na Wadau wa Maendeleo kushirikiana ili kudhibiti Vitendo vya Rushwa kwa lengo la kujenga Taifa imara na lenye uzalendo.
Aidha, Simbachawene amesema kuwa Mapambano ya Rushwa hayawezi kufanya na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pekee yake, bali wadau wote huku akiwataka viongozi wa Dini kukemea Vitendo vya Rushwa kupitia nyumba za Ibaada.
Simbachawene ameyasema hayo leo wakati akizundua Jengo la Ofisi za TAKUKURU mkoa wa Simiyu huku akiwasisitiza wananchi kuendelea kulinda amani ya Tanzania ili kuwa na nchi salama yenye Ustawi na Maendeleo Kwa watu wote.
Aidha ameitaka Taasisi hiyo kudhibiti Rushwa ndogondogo ambazo zimekuwa kero Kwa wananchi hasa kwenye vituo vya kutolea maamuzi ikiwemo vituo vya Polisi, masoko, vituo vya afya na maeneo mengine ya kutolea huduma za kijamii.
"Rushwa inapofusha, ili tuwe na Jamii yenye ustawi ni lazima Kupambana na kansa ya Rushwa kwa kuweka jitihada bila kudharau Rushwa yoyote...Rushwa ndogondogo ni mbaya na zinakera na kuumiza wananchi, taasisi tushughulike kero hizi" amesema Waziri huyo.
Amefafanua kuwa Vitendo vya Rushwa vinauwa ustawi wa wananchi, hivyo ni lazima viongozi waitafsiri kwa namna inavyoumiza.wananchi katika ngazi fulani za utoaji wa huduma.
Amesema serikali inaendelea kushugulika na kero za wananchi hasa kwenye Mapambano ya Rushwa huku akiwataka watumishi wa Taasisi hiyo kufanya kazi kwa weledi hasa kuelekea kipindi hiki Cha Uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2025.
"Tunawapongeza TAKUKURU mlivosaidia ustawi wa Jamii..Mapambanonya Rushwa hayawezi kufanywa na TAKUKURU pekee yao, tukishiikiana wote, adui tutapambana nae na Viongozi wa Dini mnayo dhima na jukumu la kukemea Rushwa kupitia Misikiti na Makanisa" amesema.
Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU, Chrisipin chalamila amewataka Wananchi kuendelea kufichua Vitendo vya Rushwa ili kuwa na nchi salama.
Awali, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu, Manyama Tungaraza amesema kuwa ujenzi wa Jengo la Ofisi za TAKUKURU umekamilia Kwa gharama ya shilingi Mil.640 ili kusogeza na kurahisisha utoaji wa huduma
Alieleza kuwa mlalamiko ya Rushwa yanatekelezwa. kwa ufasaha Kwa Mujibu wa madawati ya uchunguzi, uelimishaji umaa, uzuiaji Rushwa pamoja na huduma za Kisheria
""umejikita zaidi katika uzuiaji wa Vitendo vya Rushwa Kwa Kufanya ufuatiliaji wa matumizi miiradi ya serikali ambapo wananchi waibua kero mbalimbali ambazo zikiachwa zinaweza kusababisha kuwepo kwa Vitendo vya rushwa na Takukuru Kwa kushirikiana na wadau tunatoa majibu ya kero" amesema.
Mwisho.
Post a Comment