MAGEMBE NONI ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA GEITA MJINI.


 



Na Mwandishi wetu, Geita.



MWANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Magembe Noni, ambaye ni mzaliwa wa Mkoa wa Geita, amechukua rasmi fomu ya kuwania uteuzi wa kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Geita Mjini. 


Magembe Noni ni mtaalamu wa Jiolojia, mwenye uzoefu mpana katika masuala ya Uongozi, Utawala, Usimamizi na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.


Kada huyo ni mzalendo ambaye ameamua kutumia maarifa na muda wake kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa, ikiwa ni pamoja na kushiriki katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ya serikali.


Miongoni mwa miradi hiyo ya kimkakati ni pamoja na Usimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) ambao umekamilika kwa mafanikio makubwa, pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo Mkubwa wa Kilovoti 400 (400kV) unaounganisha Gridi ya Taifa ya Tanzania na ile ya Zambia kupitia Mradi wa TAZA.


Baada ya mchango wake mkubwa kwa Taifa,  Magembe amerudi nyumbani kwao Geita, akiwa na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa jimbo lake kama Mbunge, ikiwa atapewa ridhaa na chama chake na baadaye kuungwa mkono na wananchi.


Katika maelezo yake kwa Waandishi wa Habari, amesema lengo lake ni kushirikiana na wananchi kuharakisha maendeleo, kuimarisha uwakilishi wa kweli, na kutumia ujuzi alionao kushirikiana na serikali katika kuleta mabadiliko chanya kwa jamii ya Geita Mjini na Taifa kwa ujumla.



Mwisho.







Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم