MKURUGENZI NDABHONA AWATAKA WATUMISHI KUZINGATIA MAADILI, KUPENDANA.

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Bariadi Mkoani Simiyu, Idd Ally Ndabhona, akiongea na watumishi wa kada ya Ualimu katika ukumbi wa Halmashauri hiyo ulioko Nyaumata.


Na Mwandishi wetu.


MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Bariadi Mkoani Simiyu, Idd Ally Ndabhona amewataka Watumishi waliopata ajira hivi karibuni katika idara ya Elimu kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma.


Aidha amewataka kuwa na nidhamu ambayo itasaidia katika kuongeza chachu ya ufundishaji na kuleta matokeo chanya katika ufaulu wa wanafunzi.


Ndabhona ameyasema hayo Julai 10, 2025 wakati akifungua mafunzo maalumu Kwa ajira kanda ya ualimu ambao wamepatiwa mafunzo elekezi kabla ya kuanza  kutekeleza majukumu yao ya kazi katika vituo mbalimbali walivyopangiwa yaliyofanyika katika ukumbi huo ulioko Nyaumata.


Aidha Ndabhona ameongeza Kwa kuwataka kuachana na mikopo umiza ambayo imekuwa ikitolewa na imekuwa ikileta athari kwao huku akisisitiza masuala mbalimbali ikiwemo kuwa na mbinu bora ya ufundishaji ambayo itawafanya wanafunzi kufurahia masomo yao.


Amewataka pia kuzingatia suala ya mavazi kuhakikisha wanakuwa nadhifu na kujenga taswira iliyobora Kwa jamii inayowazunguka.


Hata hivyo amesema Halmashauri itaendelea kuwaheshimu na kuwasaidia katika masuala yote ili kuwe na mazingira rafiki na mazuri ambayo yataleta tija katika ufanyaji kazi wao katika maeneo mbalimbali.


Naye Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CTW), Wilaya ya Bariadi, Magambo Petro amemshukuru Mkurugenzi kwa namna ambayo ameonyesha Dira ya ushirikiano na matumaini Kwa waajiriwa hao wapya huku akiahidi kuendelea kuwasaidia walimu hao katika Nyanja mbalimbali. 


Mwisho.











Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم