TINA CHENGE AONGOZA KURA ZA UBUNGE VITI MAALUMU SIMIYU.

Tina Chenge.

 

Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


MJUMBE wa Baraza la Umoja wa Wanawake (UWT) Taifa, Tina Chenge ameongoza kura za Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu kwa kupata kura 631, akifuatiwa na Ester Midimu aliyepata kura 500.


Akitangaza Matokeo hayo, Kamisaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo AnnaMringi Macha amesema kuwa katika kura hizo hakuna Mashindi bali ni kura za maoni ambazo zitatumiwa kuendeleza michakato mingine ndani ya CCM.


"Wapiga kura walikuwa 1053, kura zilizopigwa 1034, kura zilizoharibika 5, kura halali 1029...Grace Balele kura 34, Jane Masanja 50, Limi Kilalo 60, Rosemary Ng'hwani 186, Minza Mjika 292, Caritas Machupa 312, Ester Midimu 500 na Tina Chenge 631" amesema Macha.


Mwisho.

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post