Mhandisi Kundo Mathew.
Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
ALIYEKUWA NAIBU Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew ameongoza katika Uchaguzi wa kura za maoni wa kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Bariadi Mjini kwa kupata kura 2,520, akifuatiwa na aliyekuwa Mbunge wa Vijana Mkoa wa Simiyu Lucy Sabu aliyepata kura 996.
Akitangaza Matokeo hayo, Katibu wa CCM wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Ibrahimu Kijanga amesema kuwa Uchaguzi huo umefanyika kwa amani na Utulivu na kuwataja Wagombea wengine ambao ni Heri Nengelo aliyepata kura 85 pamoja na Dk. Buyiki aliyepata kura 14 na kwamba kura zilizopigwa zilikuwa 3657, kura halali 3615 na zilizoharibika 42.
Mwisho.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق