JAMBO AONGOZA KURA ZA MAONI JIMBO LA MEATU.

Khamis ashinda kwa kishindo kura za maoni Jimbo la MeatMeatu.

Salum Khamis almaarufu "Jambo".


Na COSTANTINE MATHIAS, Meatu.


MFANYABIASHARA Maarufu katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Salum Khamis almaarufu "Jambo" ameongoza kushinda kura za maoni kwa nafasi ya Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Meatu Mkoani Simiyu kwa kupata kura 5,752 huku akimshinda aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Leah Komanya aliyepata kura 370.


Akitangaza Matokeo hayo, Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa CCM wilaya ya Meatu, Naboth Manyoni amesema kuwa uchaguzi wa ndani ya Chama umefanyika kwa amani na Utulivu.


Manyonyi amemtaja Luhende Hunge aliyepata kura 632 kuwa Mshindi wa pili huku Wagombea wengine waliokuwa kwenye kinyang'anyiro hicho ni Robert Machibya aliyepata kura 146, Oscar Paul 91 na Renatus Philbert kura 33.


Mwisho.



Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post