Na COSTANTINE MATHIAS,.Busega.
ALIYEKUWA Mbunge Jimbo la Busega Simon Songe ameongoza kuwa Mshindi wa kura za maoni ya Ubunge wa Jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata kura 7,787 sawa na asilimia 72 ya kura zote akifuatiwa na Dk. Raphael Chegeni aliyepata kura 1,406.
Akitangaza Matokeo ya kura hizo, Mkurugenzi wa Uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu wa CCM wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, Steven Koyo amesema kuwa Uchaguzi umefanyika vizuri ambapo kura zilizopigwa zilikuwa 10,781, kura halali 10,526 na zilizoharibika 255.
Amewataja Wagombea wengine kuwa ni Francis Nanai aliyepata kura 417, Buluba Mabelele 392, Feysal Mohammed 234, Mahaja Nduta 202 na Semistatus Mashimba kura 88.
Mwisho.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
Post a Comment