Na COSTANTINE MATHIAS, Kisesa-Simiyu.
MUSA Mbuga ametangazwa kuongoza kura za maoni katika nafasi ya Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Jimbo la Kisesa wilayani Meatu Mkoani Simiyu kwa kupata kura 3,733.
Akitangaza Matokeo hayo, Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa CCM wilayani Meatu, amesema kuwa Uchaguzi huo wa ndani ya Chama umefanyika kwa kufuata misingi na kanuni huku akiwataja Wagombea wengine ambao ni Lusingi Sita aliyepata kura 1,434, Shilinde Gumada 319, Gambamala Marco 255, Elias Joseph 101, Dk. Madili sayi 15 na Joeli Mboyi 37.
Mwisho.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق