Na Mwandishi wetu.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Tuzo ya Rais ya Kimataifa ya Wabunifu wa Mabadiliko katika sekta ya Maji 2025 (Presidential Global Water Changemaker Award 2025), heshima kubwa inayotolewa na Taasisi ya Maji (Global Water partnership) Kwa ushirikiano na Umoja wa Afrika.
Tuzo hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Botswana, Duma Boko ambaye ni Mwenyekiti wa Tuzo za Rais za Kimataifa za Wabunifu wa Mabadiliko katika sekta ya Maji 2025, ambapo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia, tuzo hiyo umepokelewa na Balozi James Bwana, Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini.
Aidha, tuzo hiyo imetolewa katika Mkutano wa kilele wa Uwekezaji katika sekta ya Maji wa AU-AIP 2024, ulioanza jijini Cape Town, Afrika Kusini na unatarajia kumalizika August 15, 2025.
Global Water Partnership imetambua uongozi bora na jitihada za mageuzi za Rais Samia katika sekta ya Maji, ikiwemo Uwekezaji Mkubwa katika miundombinu ya Maji, upanuzi wa huduma ya Maji kote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mikakati bunifu ya ufadhili kama vile hati fungani ya kijani (Green Bond) iliyotolewa na Mamlaka ya Maji ya Tanga chini ya Wizara ya Maji.
Mwisho.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com
إرسال تعليق