MIRADI YA SHILINGI BIL. 1.4 KUFIKIWA NA MWENGE WA UHURU BUSEGA.

 

MKUU wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga (kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Busega, Faiza Salum.



Na Mwandishi wetu.


MWENGE wa Uhuru 2025, umeingia katika wilaya ya Busega Mkoani Simiyu ukitokea wilaya ya Bariadi Mkoani humo, ambapo utakimbizwa kilometa 54.


Mkuu wa Wilaya ya Busega Faiza Salum ameupokea mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga. 


Ukiwa wilaya ya Busega, mwenge huo utakagua, Kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Bil. 1.4


Mwisho.

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم