Mtoto aliyefanyiwa ukatili na Baba yake anayedaiwa kuwa ni Askari Polisi. |
Na Derick Milton Bariadi.
Mtoto mmoja (Jina linahifadhiwa) mwenye umri wa
miaka 7 anayesoma katika Shule moja ya shule binafsi ya mjini Bariadi Mkoani
Simiyu amefanyiwa kitendo Cha ukatili wa kipigo na baba yake kwa madai kuwa
hajui kusoma na kuandika.
Taarifa ambazo hajidhibitsihwa ni kuwa Baba wa
mtoto huyo ni Askari Polisi kituo cha Polisi Bariadi.
Baada ya uwepo wa taarifa za mtoto huyo, Mwandishi wa Habari hii alifika Hospitali ya Mji wa Bariadi (Somanda) na kukuta mtoto huyo
akipatiwa matibabu.
Mtoto huyo alikutwa na majeraha sehemu za mgongo,
kichwa na masikioni ambapo imeonekana pia kuwa alikuwa na majeraha makubwa
ambayo ni mapya na mengine ya muda mrefu.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji wa Bariadi (Somanda),
Dr. Emmanuel Costantine aliwaambia waandishi wa habari kuwa January 19, Majira
ya saa 4:00 asubuhi walimpokea mtoto huyo kwa ajili ya matibabu.
" Tulimpokea mtoto huyu akiwa na majeraha
mapya na ya zamani (anataja jina lake), ni wa kiume miaka 7 na mkazi wa malambo
anasoma darasa la 1 shule ya msingi (anaitaja) amelazwa wodi ya watoto na
anaendelea na matibabu" anasema Dr. Costantine.
Mama mlezi wa mtoto huyo, (jina limahifadhiwa)
mkazi wa malambo amesema mtoto huyo alipigwa na baba yake ambaye alimtaja kuwa ni
askari Polisi kwa kosa la kutokuandika shuleni.
Anasema
mtoto huyo alipigwa na baba yake siku ya jumapili (January 15, 2023), na
kwamba walimpeleka shuleni siku ya Alhamisi ambapo baada ya walimu kumdadisi
ilibidi aeleze ukweli.
"Naishi pamoja na mwanaume huyo ambaye alimpiga,
mimi ni mke wake na huyo mtoto siyo wa kwangu bali ni mtoto wa mke mwenzagu ….
Nami sikufurahishwa na kitendo hicho" anasema ….
Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi ambako mtoto huyo
anasoma (jina linahifadhiwa) alisema mtoto huyo alikuwa amesajiliwa kusoma
darasa la kwanza katika Shule hiyo.
Anasema
Mahudhurio ya kijana huyo yalikuwa hafifu, Kwani siku ya jumatatu,
jumanne na jumatano hakuhudhuria masomo.
"aliletwa na mama yake wa kambo, akiwa
amechelewa saa za masomo, Mwalimu alimwona haandiki, hana raha, alipomuuliza,
akasema..." Anaeleza Mwalimu Mkuu
"Mwalimu
wa darasala alichukua uhamuzi wa kumuita mwalimu mlezi (patron),
Wakamwingiza chumba maalum kumkagua, wakakuta mtoto huyo ana majeraha
yasiyokuwa ya kawaida"
Anasema, baada ya walimu kuona Hali hiyo, walimwita
Mwalimu Mkuu na bahati nzuri mama mlezi alikuwa Bado yuko shuleni ambapo
walimbana na kuwaeleza ukweli kuwa kapigwa na baba yake mzazi kwa kutumia waya.
"Niliitwa, tukambana yule mama wa kambo, akakiri
kuwa alipigwa na baba yake kwa waya, akasema anampiga sababu
anamfundisha,.."
Mwalimu Mkuu huyo amesema kuwa walimchukua mtoto
huyo, mama mlezi pamoja na mwalimu mlezi kuelekea Kituo Cha polisi mjini
Bariadi, lakini wakiwa njiani alipigwa simu na baba yake na mtoto juu ya hali
ya mtoto, ambapo Baba mzazi limtaka Mwalimu Mkuu huyo wayamalize na asimpeleke
mtoto kituo cha Polisi.
" Wakati tunaelekea Kituoni, Baba wa mtoto
aliniomba msamaha kwa njia ya simu akinitaka tuyamalize, nami nilikataa
kutokana na hali ya mtoto alivyokuwa ameumia”
Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii katika
Halmashauri ya Mji wa Bariadi Janeth Jackson amekiri kupata tukio hilo huku akieleza
kuwa kesi imesharipotiwa jeshi la Polisi.
"Sisi kama Ustawi wa jamii tunahusika zaidi
na mtoto Kwa sababu ni kosa ambalo kalifanya baba na kesi yake iko Polisi na
sisi tunahakikisha mtoto anapata matibabu hospitalini" amesema na
kuongeza.
"Kuhakikisha anapona majeraha yake na pia
kumtafuta mtu stahiki ambaye atamlea na kuhakikisha Ulinzi na Usalama
wake"
Hata hivyo taarifa zilieleza kuwa Baba mzazi wa
mtoto huyo alikamatwa na kuwekwa rokapu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Blasius Chatanda alipotafutwa
kuzungumzia tukio hilo hakusema chochote.
MWISHO.
إرسال تعليق