MBUNGE NYONGO AJIVUNIA MAFANIKIO JIMBONI.


Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki,Stanslaus Nyongo akizungumza na wananchi kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Maswa kuelezea kazi alizofanya na atakazofanya Kwa mwaka huu.

 


Baadhi ya Viongozi wa CCM na Serikali wa Wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu waliohudhuria mkutano WA Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki,Stanslaus Nyongo(mwenye shati jeupe)wakifurahia jambo.


Na Samwel Mwanga,Maswa.

 

MBUNGE wa jimbo la Maswa Mashariki katika mkoa wa Simiyu,Stanslaus Nyongo amesema kwamba amefanikiwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo katika sekta za afya, elimu, maji na barabara jimboni humo tangu alipochaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo Hilo mwaka 2020.

 

Alisema hayo wakati akihutubia mkutano hadhara iliyofanyika mjini Maswa ikiwa ni moja ya mikutano yske ya kusikiliza kero za Wananchi sambamba na kueleza shughuli zilizofanyika na ziyakazofanyika Kwa mwaka huu.

 

Alisema kuwa kwa kipindi cha  miaka miwili tangu achaguliwe kuwa mbunge serikali imeleta fedha zaidi ya Sh Bilioni 30 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.

 

Alisema kuwa kwa sasa serikali inayoongozwa na Rais  Dkt Samia Suluhu imeleta fedha hizo katika jimbo hilo kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari,Vituo vya afya,Miradi ya Maji na Miundombinu mbalimbali ya barabara.

 

Nyongo aliitaja miradi mingine ya kimaendeleo iliyotekelezwa na inayotekelezwa kwa sasa chini ya uongozi wake kuwa ni ujenzi wa barabara za lami,mitaro ya Maji ya mvua na uwekaji wa taa za barabarani katika mitaa ya mji wa Maswa,Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya  Nyongo katika Kata ya Nyalikungu , Kituo cha Afya cha Ipililo na Ukarabati wa soko Kuu la mjini humo.

 

Miradi mingine inayotekelezwa ni pamoja na miradi ya maji ikiwemo ya Ujenzi wa tenki la kuhifadhi Maji Lita Milioni moja katika kilima Cha Nyalikungu,Ujenzi wa tenki la kuhifadhi Maji Lita Milioni mbili katika Kijiji Cha Hinduki,Ujenzi wa vituo vitano vya kuchotea maji katika kitongoji cha Jashimba na mradi wa maji katika Kijiji cha Mwashegeshi.

 

Nyongo aliitaja miradi mingine ni pamoja miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Vyoo katika shule mbalimbali za sekondari na shule za Msingi katika jimbo hilo na ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Mwagala.

 

“Kwa muda wote tangu mnichague mwaka 2020, nimekuwa na harakati za kusimamia na kuchochea utekelezwaji wa miradi ya maendeleo na hata ninyi ni mashahidi, maana mmekuwa mkishiriki kwa namna moja au nyingine katika kutekeleza miradi hiyo,” alisema.

 

Pia alisema kuwa katika jimbo hilo vijiji vyote na taasisi zote za serikali zimepatiwa huduma za nishati ya umeme ili kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma hiyo muhimu kwa maisha ya kila siku hivyo vitongoji vyoye navyo vitapata umeme.

 

Pia aliwaomba viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)kuanzia ngazi ya tawi hadi Kata kuhakikisha wanakuwa wasimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali katika maeneo yao.

 

"Niwaombe Viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya Tawi hadi Kata hakikisheni hii miradi inayoletwa kwenye maeneo yenu na serikali mnaisimamia vizuri maana ni yenu,"alisema.

 

Aidha alisema kuwa haogopi kwa wapinzani kuja kufanya mikutano kwenye Jimbo hilo kwani amefanya kazi Kwa kipindi kifupi na ifikapo mwaka 2025 atakuwa hana deni Kwa Wananchi waliomchagua kwani yeye ndiye atawadai kura.

 

Mkuu wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge alitumia fursa hiyo kumshukuru Mbunge huyo kwa kuhakikisha anasukuma fedha huko bungeni za miradi mbalimbali inayokuja katika Jimbo hilo na wilaya Kwa ujumla na yeye amekuwa akizisimamia Ili ziweze kufanya kazi zilizokusudiwa.

 

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم