Sehemu ya Bwawa la New Sola katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu likiwa limejaa kufuatia watu kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye hifadhi ya bwawa hilo |
Na
Samwel Mwanga,Maswa.
BWAWA
la Maji la New Sola (maarufu bwawa la Zanzui )lililo katika wilaya ya Maswa
mkoa wa Simiyu limejaa maji ambayo yamezidi uwezo wa bwawa hilo na sasa
maji yaliyozidi yanapita kwenye utoro wa maji wa bwawa hilo kuelekea mto
Simiyu.
Bwawa
hilo ndicho chanzo kikuu cha maji kwa wakazi wapatao 120,000 wa mji wa
Maswa na vijiji 12 vinavyotumia maji hayo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Maswa (Mauwasa) Mhandisi
Nandi Mathias amesema kuwa bwawa hilo limejaa maji kutokana na Mkuu wa wilaya
hiyo,Aswege Kaminyoge na Kamati mzima ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo
kuwataka kuhifadhi vyanzo vya Maji vinavyoingiza Maji kwenye bwawa hilo.
Amesema
kuwa walielekeza nguvu kubwa kulinda hifadhi hasa mto Sola kwa kuzuia wananchi
waliojitokeza kufanya shughuli za kilimo kwenye hifadhi hiyo mwezi
Disemba mwaka jana.
Mhandisi
Nandi amesema kuwa kutoka na jitihada hizo za kulinda chanzo cha mto huo ambao
unachangia asilimia 75 ya maji yote yanayoingia katika bwawa hilo matokeo
yake kwa mvua zilizonyesha Mwezi Disemba mwaka jana hadi kufikia Januari 18
mwaka huu,bwawa la New Sola lenye uwezo wa kujaa lita Bilioni 5 za maji limejaa
zaidi ya hapo.
"Mto
Sola ndiyo unaingiza Maji asilimia 75 kwenye bwawa letu la New Sola ndiyo maana
Mkuu wa wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ilitutaka kuwekwa nguvu
kubwa Kwa kusaidiana nao kuhakikisha chanzo hicho kinalindwa Kwa gharama
zozote,"amesema.
Amesema
kwa sasa bwawa limefikia kikomo chake na maji yaliyozidi yanaondoka kupitia utoro
wa maji wa bwawa hilo na kuelekea mto Simiyu unaopeleka Maji yake katika Ziwa
Victoria Ili kuweza kunusuru uhai wa Bwawa la New Sola.
Mhandisi
Nandi ametoa wito kwa Wananchi wa vijiji vinavyolizunguka bwawa hilo kuendelea
kutunza Mazingira ya hifadhi ya bwawa hilo sambamba na mito
inayotiririsha maji kuelekea kwenye bwawa la New Sola ukiwemo mto
Mwakungwe na mto Gasela.
Aidha
ameishukuru serikali ya awamu ya sita baada ya kulipa fidia kwa wananchi
wa Kijiji cha Zanzui waliokuwa na maeneo ya kulima katika hifadhi
ya bwawa hilo na kupisha chanzo cha maji kwa sasa bwawa lina uhakika wa
kuhifadhi maji takribani meta za ujazo million 5 .
Mhandisi
Nandi pia ameishukuru serikali ya wilaya ya Maswa inayoongozwa na Mkuu wa
wilaya hiyo,Aswege Kaminyoge kwa kuendeleza usimamizi madhubuti wa vyanzo
vya maji ukiwemo mto Sola.
Pamoja
na jitihada hizo zinazofanywa na Serikali ya wilaya na Mauwasa kulinda hifadhi
ya bwawa hilo bado wapo baadhi ya wafugaji wachache wamekuwa wakiingiza mifugo
yao bwawani.
Mkuu
wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge amesema kuwa vyanzo vya Maji vikitunzwa na
kuhifadhiwa vizuri vitasaidia vizazi vijavyo na hivyo kuwataka Viongozi wa
vijiji vinavyolizunguka bwawa hilo kuhakikisha hakuna wafugaji wanaopeleka
mifugo kwenye bwawa hilo.
"Faida
ya kutunza na kuhifadhi vyanzo vya Maji ndiyo hii tumeiona maana bwawa limejaa
Maji kabla hata ya mvua za masika hivyo tuendeleze utamaduni huu wa kutunza
Mazingira na wale wachache wanaoingiza mifugo ndani ya bwawa naagiza viongozi
wa maeneo hayo kuhakikisha jambo hilo linaachwa mara mara moja,"amesema.
MWISHO.
Post a Comment