Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki,Stanslaus Nyongo akizungumza na wananchi kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Maswa kuelezea kazi alizofanya na atakazofanya Kwa mwaka huu. |
Baadhi ya Viongozi wa CCM na Serikali wa Wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu waliohudhuria mkutano WA Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki,Stanslaus Nyongo(mwenye shati jeupe)wakifurahia jambo. |
Na Samwel Mwanga,Maswa.
MBUNGE wa jimbo la Maswa Mashariki katika mkoa wa
Simiyu,Stanslaus Nyongo amesema kwamba amefanikiwa kutekeleza miradi mingi ya
maendeleo katika sekta za afya, elimu, maji na barabara jimboni humo tangu
alipochaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo Hilo mwaka 2020.
Alisema hayo wakati
akihutubia mkutano hadhara iliyofanyika mjini Maswa ikiwa ni moja ya mikutano
yske ya kusikiliza kero za Wananchi sambamba na kueleza shughuli zilizofanyika
na ziyakazofanyika Kwa mwaka huu.
Alisema kuwa kwa kipindi cha miaka miwili tangu achaguliwe
kuwa mbunge serikali imeleta fedha zaidi ya Sh Bilioni 30 kwa ajili ya miradi
mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.
Alisema kuwa kwa sasa serikali inayoongozwa na Rais Dkt
Samia Suluhu imeleta fedha hizo katika jimbo hilo kwa ajili ya ujenzi wa shule
za sekondari,Vituo vya afya,Miradi ya Maji na Miundombinu mbalimbali ya
barabara.
Nyongo aliitaja miradi
mingine ya kimaendeleo iliyotekelezwa na inayotekelezwa kwa sasa chini ya
uongozi wake kuwa ni ujenzi wa barabara za lami,mitaro ya Maji ya mvua na
uwekaji wa taa za barabarani katika mitaa ya mji wa Maswa,Ujenzi wa Shule mpya
ya Sekondari ya Nyongo katika Kata ya Nyalikungu , Kituo cha Afya cha
Ipililo na Ukarabati wa soko Kuu la mjini humo.
Miradi mingine inayotekelezwa ni pamoja na miradi ya maji
ikiwemo ya Ujenzi wa tenki la kuhifadhi Maji Lita Milioni moja katika kilima
Cha Nyalikungu,Ujenzi wa tenki la kuhifadhi Maji Lita Milioni mbili katika
Kijiji Cha Hinduki,Ujenzi wa vituo vitano vya kuchotea maji katika kitongoji cha
Jashimba na mradi wa maji katika Kijiji cha Mwashegeshi.
Nyongo aliitaja miradi mingine ni pamoja miradi ya ujenzi wa
vyumba vya madarasa na Vyoo katika shule mbalimbali za sekondari na shule za
Msingi katika jimbo hilo na ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika shule
ya sekondari Mwagala.
“Kwa muda wote tangu mnichague mwaka 2020, nimekuwa na harakati
za kusimamia na kuchochea utekelezwaji wa miradi ya maendeleo na hata ninyi ni
mashahidi, maana mmekuwa mkishiriki kwa namna moja au nyingine katika
kutekeleza miradi hiyo,” alisema.
Pia alisema kuwa katika jimbo hilo vijiji vyote na taasisi zote
za serikali zimepatiwa huduma za nishati ya umeme ili kuhakikisha kila
mwananchi anafikiwa na huduma hiyo muhimu kwa maisha ya kila siku hivyo
vitongoji vyoye navyo vitapata umeme.
Pia aliwaomba viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)kuanzia ngazi
ya tawi hadi Kata kuhakikisha wanakuwa wasimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa
na serikali katika maeneo yao.
"Niwaombe Viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya Tawi hadi Kata
hakikisheni hii miradi inayoletwa kwenye maeneo yenu na serikali mnaisimamia
vizuri maana ni yenu,"alisema.
Aidha alisema kuwa haogopi kwa wapinzani kuja kufanya mikutano
kwenye Jimbo hilo kwani amefanya kazi Kwa kipindi kifupi na ifikapo mwaka 2025
atakuwa hana deni Kwa Wananchi waliomchagua kwani yeye ndiye atawadai kura.
Mkuu wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge alitumia fursa hiyo
kumshukuru Mbunge huyo kwa kuhakikisha anasukuma fedha huko bungeni za miradi
mbalimbali inayokuja katika Jimbo hilo na wilaya Kwa ujumla na yeye amekuwa
akizisimamia Ili ziweze kufanya kazi zilizokusudiwa.
Post a Comment