Na
Derick Milton, Tabora.
Mshindi wa shindano la NMB MastaBata Kote-Kote linaloendeshwa
na Benki ya NMB Emmanuel Marumbo kutoka Mkoani Tabora amekabidhiwa rasmi Pikipiki
yake leo aina ya Boxer.
Mshindi huyo wa jumla aliyepatikana katika droo ya
nane ya shindano hilo iliyofanyika wiki iliyopita Mkoani Tanga, amekabidhiwa
zawadi yake na Meneja Masoko NMB Kanda ya Magharibi Trifon Malkiory.
Hafla ya kumkabidhi zawadi hiyo imefanyika leo kwenye
Tawi la NMB Mihayo mjini Tabora, ambapo kabla ya kumkabidhi zawadi mshindi
Meneja huyo aliendesha droo ya tisa ya shindano hilo kwa wiki hii.
Katika droo hiyo iliyosimamiwa na Mkaguzi kutoka
Bodi ya michezo ya kubahatisha Goodluck Msomigulu, amepatikana Aidan Stephen
Lukindo kutoka Mkoani Morogoro na kuwa mshindi wa jumla wiki hii na
kujinyakulia zawadi ya Pikipiki aina ya Boxer.
Aidha droo hiyo imewapata washindi wengine 75
ambao wamejishindia kiasi cha Sh.100,000 kila mmoja kupitia shindano hilo.
Meneja Masoko Trifon amesema kuwa NMB imekuwa
ikiendesha shindano hilo ukiwa ni mwaka wa nne tangu limeanza, ambapo linalenga
kuhamasisha wateja wake kutumia kadi na Mastercard QR.
Amesema kuwa NMB inaendesha shindano hilo kama
njia ya kurudisha faida kwa wateja wake, ambapo washindi ujishindia zawadi
mbalimbali zikiwemo fedha taslimu, pikipiki pamoja na safari ya kuelekea Dubai
kwa siku nne.
“ Niwakumbushe pia zaidi ya Sh. Milioni 300
zitatolewa kama zawadi kwa washindi 854, na kampeini inaendeshwa ndani ya wiki
kumi na kila wiki washindi 75 wanapokea kiasi cha sh. 100,000 na mshindi mmoja
pikipiki” amesema Malkiory.
Amewataka wateja wa Benki hiyo kuendelea kutumia
kadi zao za NMB Master Card, siyo tu kwa ajili ya kutolea pesa kwenye mashine
za ATM bali hata kwa matumizi mbalimbali ili wajishindie zawadi mbalimbali
kupitia shindano hilo.
“ wateja wetu wanaweza kufanya malipo ya skani QR
kwa kulipa mkononi katika sehemu za migahawa, supermarket, vituo vya mafuta
lakini pia hata kwenye sehemu za starehe na hata kuagiza bidhaa mbalimbali
kupitia mitandao” amesema Malkiory
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya Pikipiki
mshindi wa droo ya wiki iliyopita, Emmanuel Marumbo amesema mwanzoni hakuamini
kama kweli ameshinda zawadi hiyo licha ya kuwashirikisha wenzake.
Amesema kuwa amekuwa ni mtu wa kutumia kadi ya
benki yake kwa ajili ya manunuzi ya vitu mbalimbali, huku akibainisha kuwa huwa
hatembei na pesa taslimu bali ufanya manunuzi kwa kutumia kadi yake.
Ameishukuru benki ya NMB kwa zawadi waliyompatia
huku akibainisha kuwa itamsaidia katika shughuli zake za biashara za kila siku
anazozifanya, kwani amepata usafiri wa kurahisisha kazi zake.
Amewataka wateja wa NMB kujiwekea utaratibu wa
kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia kadi za benki, kwani kufanya hivyo kuna
usalama zaidi wa pesa lakini pia NMB kupitia shindano lake inatoa zawadi
mbalimbali.
MWISHO.
إرسال تعليق