Hivi ndivyo Konyagi feki ilivyokuwa ikitengezwa Bariadi.

 



 

Na Mwandishi wetu, Bariadi.


Leo kupitia  (simiyupresstz.blogspot.com)  tumeripoti juu ya kunaswa kwa kiwanda Bubu kilichokuwa kikitengeneza pombe kali aina ya Konyagi, kiwanda ambacho kimekamatwa katika Mtaa wa Budeka, kata ya Sima Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.

 

Kiwanda hicho kilibainika baada ya Kamati  ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Bariadi kufanya opereisheni na kukuta vijana wakiendelea na utengenezaji wa pombe hiyo kwenye nyumba moja iliyoko katika mtaa huo.

 

Hata hivyo wahusika wa kiwanda hicho bubu, walikodi moja ya nyumba katika mtaa huo na kuanza kungeneza pombe hiyo ambayo inadaiwa kutokuwa salama kwa walaji.

 

Hivi ndivyo pombe hiyo ilivyokuwa ikitengenezwa. 

 

Taarifa zinaeleza kuwa bidhaa hiyo ilikuwa ikizalishwa kienyeji licha ya kuwa na nembo halali ya Konyagi, stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), lakini pia bidhaa hiyo haina tarehe ya kuanza kutumika wala tarehe ya mwisho wa matumizi (Expire date).

 

Mbali na hilo pombe hiyo inadaiwa ilikuwa ikitengenezwa kwa kuchanganywa Maji na Spriti, ambapo wahusika walikuwa wakitafuta chupa tupu za konyagi, maboksi yenye nembo ya Konyagi, kisha kufanya mchanyiko na kupeleka sokoni.

 

Akizungumzia tukio hilo, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala wilaya ya Bariadi Nichodemus Shirima amesema wamekamata watu wawili waliokuwa katika kiwanda hicho bubu huku akibainisha kuwa pombe ambayo ilikuwa ikitengenezwa kwenye kiwanda hicho ni hatari kwa walaji.

 

“Hiki kinywaji hakijapimwa, hakina TBS, hakuna mtu anayejua kama kinywaji hiki ni sumu au laah…inaonekana kuna ulegevu katika ukaguzi mpaka watu wameamua kuanzisha viwanda bubu katika makazi ya watu lakini tunashukuru hatimaye wamebainika’’ amesema na kuongeza.



Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم