MAUWASA yaanza kutumia bei mpya za Maji Mjini Maswa.

Sehemu ya bwawa la New Sola lililoko katika wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu ambacho ndicho chanzo kikuu cha maji katika mji wa Maswa na vijiji 11 ambalo linamilikiwa na MAUWASA.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Maswa (MAUWASA) Mhandisi Nhandi Mathias (mwenye koti la drafti) akiwatisha ndoo baadhi ya wakina mama mjini Maswa.

 


Na SAMWEL MWANGA, Maswa.

 

MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Maswa (MAUWASA) iliyoko katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu imetangaza na kuanza kutumia rasmi bei zake mpya za ankra ya Maji.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo Cha Mahusiano na huduma kwa Wateja iliyothibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mauwasa, Mhandisi Nandi Mathias imeeleza kuwa mabadiliko hayo ya bei ya Maji imeanza kutumika mwezi Februari mwaka huu Ili lusaidia Kuboresha huduma ya Maji safi na salama katika mji wa Maswa na vijiji 11.

 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mabadiliko hayo ya    bei  ya maji yameidhinishwa  na Mamlaka  ya  udhibiti  wa  Nishati  na  Maji nchini Tanzania (EWURA), 

 

Imeeleza kuwa  mabadiliko  hayo  yalipaswa  kuwa yamefanyika   tangu  Julai,  2021 lakini yalichelewa  kufanyika kutokana  na  sababu ambazo  zilikuwa  nje  ya uwezo wa Mamlaka hiyo.

 

Kufuatia Mabadiliko hayo kwa sasa wateja wa manyumbani  kwa unit 1 ya  Maji ni Sh 1,900/ kutoka Shs. 1,600/ ya awali na Wakala wa Magati.(Vioski ) unit 1 ya Maji ni Sh 1,900/= kutoka Sh.1,600/- ya Awali.

 

Wale wateja wa Taasisi za Umma na binafsi Kwa sasa watalipa  unit 1 ya maji Sh 2,300/ kutoka Sh 1,900/ ya Awali,Wateja wa  kundi la biashara kwa unit 1 ya maji  watalipa Sh.2,800/ kutoka Sh 2,300/=ya Awali.

 

Wateja wa kundi la viwanda Kwa unit 1 ya maji sasa watalipa Sh.2,900/-kutoka Ile ya Sh 2,600/ na wateja wasio na mita* watatonzwa  sh 17,600/- kwa Mwezi.       

 

Pia taarifa hiyo imetoa ufafanuzi kuwa unit 1 ya maji ni sawa na ndoo 50 za maji zenye ujazo wa lita 20 kila moja.

 

Mhandisi Nandi akizungumza lwa njia ya simu amesema kuwa kwa sasa gharama pia za uendeshaji zikuwa za juu hasa kwenye kulipia umeme kila mwezi kwenye mitambo ya maji pamoja na gharama za kununulia madawa Kwa ajili ya kuyatibu Maji.

 

"Chanzo chetu kikuuu cha maji ni bwawa la New Sola hivyo Maji haya tunayasukuma kwa umeme na tunayatibu kwa madawa ili wateja wetu wapate maji safi na salama kwa gjarama kubwa hivyo ukiangalia gharama za uendeshaji na makusanyo yetu bado tunachangoto,"

 

"Licha ya wateja wetu kuonekana kushangazwa na mabadiliko hayo lakini tutatumia njiambalimba li zikiwemo vyombo vya habari,vipeperushi, Matangazo kwenye Mbao za Matangazo,Mitandao ya kijamii na number kwenye simu za mkononi kuwaelimisha wananchi hasa wateja wetu juu ya ongezeko hilo Ili kuepuka usumbufu wakati wa ulipaji wa ankra hizo za maji.

 

Baadhi ya wateja wa Mauwasa wameiomba Mamlaka hiyo kukutana nap na kuwapatia taarifa za mabadiliko hayo ya bro kuliko kukutana nayo kwenye ankra za maji za mwezi Februari.

 

Aidha wameeleza kuwa wamekuwa wakipata changamoto ya ukosefu wa Maji kufuatia miundombinu ya maji kukatwa na Wataalam wanaotengeneza barabara katika mji wa Maswa.

 

MWISHO

Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم