Moja ya nyumba ambayo iliezuliwa paa na ukuta kuanguka kufuatia mvua ya Mawe iliyoambana na upepo mkali kuonyesha katika mji wa Malampaka wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu. |
Na Samwel Mwanga,Maswa.
MVUA kubwa iliyoambatana na Mawe na upepo
imesababisha maafa ya kuezuliwa paa katika nyumba10 na kuangusha ukuta
nyumba mbili katika mji wa Malampaka wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu.
Pia watu 51 ambao ni wakazi wa kaya katika
nyumba hizo hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuezuliwa paa na kuta
kuanguka.
Kwa mujibu wa taarifa ya Afisa
Mtendaji wa Kijiji cha Malampaka,Julius Mabondo aliyoitoa Kwa Mkuu wa wilaya ya
Maswa,Aswege Kaminyoge ameeleza kuwa hakuna taarifa ya kifo katika Maafa hayo.
Amesema kuwa mvua hiyo imenyesha Februari
17 mwaka huu majira ya saa 9:00 mchana na ilidumu takribani dakika 30
Amesema licha ya mvua hiyo kuleta Madhara imesababisha
kuangusha transfoma ya Umeme ambayo ni mali ya Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini
(Tanesco) pamoja na kuathiri mazao mbalimbali yaliyoko shambani ambayo ni na
mahindi na Pamba, huku akibainisha kuwa taarifa sahihi ni kiasi gani cha hekari
kilichoathirika bado haijaandaliwa.
Amesema hadi sasa thamani ya athari
iliyosababishwa na mvua hiyo Bado haijafahamika huku tathmini ya madhara hayo
ikiendelea kufanyika.
"Mheshimiwa Mkuu wa wilaya
pamoja na Madhara haya hakuna kifo chochote
kilichoripotiwa kufuatia mvua hizo na hata tathimini ya Maafa haya bado
kufanyika hivyo ikifanyika tutajua gharama za uharibifu huu,"alisema.
Mkuu wa wilaya hiyo,Kaminyoge ambaye
alizitembelea kaya hizo zilizopata maafa hayo mbali na kuzipatia pole aliigiza
halmashauri ya wilaya ya Maswa kuhakikisha inatoa kiasi cha kilo 60 za mahindi
na mboga zikiwemo dagaa na maharage kwa kila kaya ambayo imeathirika pamoja na
kupatiwa hifadhi ya muda wakati wakiendelea na urekebishaji wa nyumba hizo.
Pia aliuagiza Uongozi wa Halmashauri hiyo
kufanya tathimini ya Maafa hayo Ili kupata gharama halisi sambamba na Idara ya
Ujenzi kuwapatia Elimu juu ya kujenga nyumba Bora ambazo zinaweza kuhimili hali
hiyo ikitokea tena.
"Mkurugenzi wa wilaya ya Maswa kwa kuwa
serikali imetuletea mahindi ya bei nafuu hakikisha Kwa msaada wa haraka hizi
kaya zote zilizokumbwa na Maafa kila moja inapata kg 60 ya mahindi pomoja na
mboga ambazo ni dagaa na maharage"
"Pia waathirika hawa wapewe hifadhi ya
muda wakati wanarekebisha nyumbani zao na tathimini ifanyike kujua gharama
halisi ya maafa hayo Ili Serikali ione namna ya kuwasaidia sambamba wataalam wa
Ujenzi toeni elimu kwa wananchi juu ya Ujenzi bora wa nyumba,"alisema.
Naye diwani wa Kata ya Malampaka,Renatus
Mashala (CCM) pamoja na kumshukuru Mkuu huyo wa wilaya kufika katika mji huo na
kujionea Maafa hayo ameishukuru serikali kwa msaada huo ambao utatolewa na
kusisitiza kuwa watazisaidia kaya hizo ili ziweze kuishi kama ilivyokuwa awali.
MWISHO.
إرسال تعليق